Tatizo la ngozi liitwalo keloids

Tatizo la ngozi liitwalo keloids

mzee wa nguna

Senior Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
138
Reaction score
136
Wadau mpo hamjambo?

Napenda kuwashirikisha katika tatizo hili linalowapata baadhi ya watu ambapo wakipatwa na jeraha hata dogo basi likipona ngozi inainuka na kuunda ngozi ngumu inayoendelea kukua bila ukomo.

Vivimbe hivi sio kansa wala havitishii uhai bali kero yake ni mabadiliko ya ngozi.

Hii husababisha usumbufu mkubwa sana na kuharibu muonekano wa ngozi ya eneo lililoathirika.

Aidha wahusika wanadai yanakuwa na muwasho wa kudumu.

Kwa mwenye utaalamu atupe dondoo tatizo hili husababishwa na nini, jinsi ya kuzuia na iwapo pana tiba ya aina yoyote hapa kwetu Tanzania ikibidi na gharama zake...

Nawasilisha.

images
images
images
images
images
 
Ina maana jf nzima hakuna. Mwenye kujua lolote kuhusu huu ugonjwa?
 
Back
Top Bottom