Tatizo la ngozi msaada unahitajika

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
4,824
Reaction score
5,587
Habari zenu ndugu zangu !bila kupoteza mda nijikite kwenye mada nimekuwa na tatizo la ngozi yangu kutokurleweka kwa mda mrefu ikiwemo kutokuwa na specific colour Mara mweupe Mara mweusi Mara mabakamabaka japo sio sana na ni baadhi ya maeneo ya mwili.

Sasa hizi siku za karibuni nimekuwa nikiwashwa sana mwili kuanzia mabegani shingo hadi mgongoni ngozi imekauka imetokeza vidude kama vibalango hata nikipaka mafuta haviishi

Sielewi tatizo nini wakuu
Mafuta nayotumiaga ni samona nishajaribu kutumia mafuta tofauti tofauti hata losheni ila naona ngozi yangu haitulii

Naombeni msaada wakuu hili tatizo ni nini na tiba yake unaweza kuwa nini?
 
fanya mpango umuone daktari bingwa wa ngozi Dermatologist na ukianza matibabu fua nguo zote ulizotumia pamoja na mashuka na mataulo uyapige pasi. Kua mvumilivu matibabu yanaweza kuwa ni ya muda mrefu.
 
Asante mkuu kwa ushauri japo naogopa sana tiba za hospital
 
Kwa hiyo ulikuja hapa ukitegemea utaalamu wa tiba mbadala?
Vyovyote ila unajua humu kuna watu wana experience na magonjwa kama ayo nipate ushauri walifanyaje mpaka wakapona ila ushauri wako ntauzingatia maana nawashwa mpaka najisikia kama homa nikijimwagia maji ndo balaa
 
Chukua alovera menya ule utando wake wa ndani ponda mpk upate mchuzi ukishaoga usiku paka sehemu zote zilizoathirika kwa muda wa wiki 3 utaniambia
 
Chukua alovera menya ule utando wake wa ndani ponda mpk upate mchuzi ukishaoga usiku paka sehemu zote zilizoathirika kwa muda wa wiki 3 utaniambia
Sawa mkuu ngoja ntaifatfa hiyo aloevera japo nilipo ni adimu kuipata na sijawai kuiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…