Tatizo la pikipiki kuzima ukiwasha taa

Tatizo la pikipiki kuzima ukiwasha taa

Amaizing Mimi

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2019
Posts
489
Reaction score
1,102
Salamu kwenu wakuu,Nina pikipiki yangu aina ya TVS 125.

Tatizo lake ni pale ninapowasha taa kubwa ya mbele baada ya dakika kadhaa pikipiki inazima, na inapotaka kuzima nikizima taa inaendelea kuwa fresh.

Nilienda kwa fundi akasema tatizo ni rectfire, nikabadili rectfire lakini tatizo likabaki pale pale. Fundi akasema huenda ni coil ndio inazalisha umeme kidogo. Nikanunua Coil mpya lakini tatizo bado halijaisha. Fundi ananiambia ni betry imechoka.

Kabla sijanunua betry naombeni ushauri wenu. Natanguliza shukrani.
 
Usinunue betri, taa inawaka bila hata uwepo wa betri kwa kutumia moto wa jiko la pikipiki na ikiwa silence mwanga utakuwa chini unapoongeza moto taa mwanga unaongezeka
 
Shida ni wiring hapo.

Ile magneto ya pikipiki ina coil zinazalisha umeme kwa matumizi tofauti kulingana na mahitaji. Umeme mwingine kwenye vifaa, Kwenye ignition system n.k

Na nina wasiwasi fundi wako umeme wa kwenda kwenye taa kubwa yeye kachukulia kwenye njia inayopeleka umeme kwaajili ya ignition hivyo ukiwasha taa kubwa unapunguza kiasi cha umeme unaoenda kwenye uchomaji na kuathiri utengenezwaji wa cheche na hapo lazima injini izime.

Ushauri: Ondoa hiyo wiring iliyoungwaungwa nunua mpya
 
Mrejesho,Nilienda kwa fundi mwingine alifanikiwa kutatua tatizo.kwa bahati mbaya sikuwepo wakati anatengeneza.
 
Back
Top Bottom