stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Wadau kwa wale madaktari au yeyote mwenye fani hii,nimegundulika nina pressure baada ya kupima mara tatu ktk siku tofauti 140/80,167/90 na163/90,nikapimwa ECG Imeonyesha normal.Daktari akaniandikia dawa za pressure,ushauri niliopata kutoka kwa mtu muathirika ni kuwa nisianze kutumia dawa ila nifanye mazoezi,nisile vitu vya mafuta na chumvi,hali naona imebadilika na najisikia vizuri baada ya kufuata masharti hayo na nilipoenda kupima hospitali nyingine baada ya 2 weeks imekuwa 150/85.Doctor alienipima akanishauri nitumie dawa zinaitwa Lasix kwa siku 10,nimeanza kutumia leo siku ya 3,ila jirani yangu hapa nyumbani naye ni doctor kanishauri nitumie dawa inaitwa Propronalin kwa siku 10 niache Lasix.Sasa mwenye uelewa mzuri naomba ushauri nitumie ipi kati ya hizo dawa?