Tatizo la pressure

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,216
Reaction score
26,225
Wadau kwa wale madaktari au yeyote mwenye fani hii,nimegundulika nina pressure baada ya kupima mara tatu ktk siku tofauti 140/80,167/90 na163/90,nikapimwa ECG Imeonyesha normal.Daktari akaniandikia dawa za pressure,ushauri niliopata kutoka kwa mtu muathirika ni kuwa nisianze kutumia dawa ila nifanye mazoezi,nisile vitu vya mafuta na chumvi,hali naona imebadilika na najisikia vizuri baada ya kufuata masharti hayo na nilipoenda kupima hospitali nyingine baada ya 2 weeks imekuwa 150/85.Doctor alienipima akanishauri nitumie dawa zinaitwa Lasix kwa siku 10,nimeanza kutumia leo siku ya 3,ila jirani yangu hapa nyumbani naye ni doctor kanishauri nitumie dawa inaitwa Propronalin kwa siku 10 niache Lasix.Sasa mwenye uelewa mzuri naomba ushauri nitumie ipi kati ya hizo dawa?
 
Umepokea ushauri tofauti toka kwa madaktari wawili bado unataka nasisi tusio madaktrai kukushauri? Kujua chanzo kinachoamsha ni muhimu kuliko hivyo vidonge
 
Pamoja na kuwa hivo ushaonesha pressure yako iko juu chamsingi kwa Sasa tumia DAWA ya kushusha afu ukapime ikiwa imeshuka uanze mazoezi kupunguxa mwili na punguza vyakula vya chunvi nyingi sukari nyingi na mafuta mengi tumia hivo vitu kwa kiasi kdg sana
 
Sawa mkuu dulao ni ipi nitumie kati ya hizo dawa?
 
Last edited by a moderator:
Hiyo proplonalin, kuna niphedipine zipo nyingi tu utakayo andikiwa
 
Sawa mkuu dulao ni ipi nitumie kati ya hizo dawa?

Stephot kuna kosa kubwa unalolifanya,nalo ni kuchanganya madaktari. Acha hiyo mara moja stick kwa daktari mmoja tena awe daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na si General Physician.

Mimi pia nilifanya makosa kama hayo unayotaka kufanya na imenichukua miaka mingi sana. Ingawaje ugonjwa wangu haukuwa mkubwa kihivyo.

Stick to the rules. Usile chumvi mbichi (Table salt) na vingine utakavyokatazwa na daktari. Pia kama unatumia pombe anza kupunguza sana kiwango unachokunywa ukielekea kuacha.

Mimi nimepima pressure kila ninpokuwa nimelala nimekunywa nakuta iko juu sana tofauti na siku nisipogusa kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana ndugu Mrigariga kwa ushauri wako,mpaka sasa niko kwenye hayo masharti na ninayafuatilia kwa makini,na tayari nimeshaona changes kubwa sana,nimeamua kuacha kabisa pombe na nimeonywa pia na wagonjwa kadhaa wa pressure kutokubali kuanza kutumia hizo dawa mapema.Niko kwenye program ya kupunguza uzito na mpaka sasa nimeshakata kilo 2 kwahiyo nafikiri nitakapopima next time nitakuwa vizuri sana.Nilicho observe ni kuwa chest pain imeisha kabisa,napata usingizi vizuri,heart pound imekata najihisi vizuri kwa kweli
 
Last edited by a moderator:
jf watakuua mkuu mziizimkavu ndie dkwetu sijui kamakarudi likizo,,else rudia hao kama watakupawazo tofauti...sipendi kukuita rip via jf mapema una nguvu,,punguza na mlo wa kitandani pia kama ni 1*3 nemda 1*2,,ikiwa bado 1*1
 
mriga vipi round za bed aziongezi hii mpwa??msaidiekwahiki pia
 
Tumia hizo dawa ulizoandikiwa kwanza,halafu usile chumvi nyingi,usinywe vinywaji vyenye caffein,fanya mazoezi,pia jitahidi usipate stress,Pressure ni mbaya sana,na ni silent killer,inaondoa kuilaini kabisa,watu wanabaki wanashangaa tu ,tulikuwanae jana na nini na nini.
 
Madkatari woye ni agents wa wauza dawa. Wanakimbilia tu dawa wanazojua. Fanya hivi kunywa kitunguu swaumu punje 3 ukiweza ponda ponda.Siku3 kapime uonea matokeo
 
Madkatari woye ni agents wa wauza dawa. Wanakimbilia tu dawa wanazojua. Fanya hivi kunywa kitunguu swaumu punje 3 ukiweza ponda ponda.Siku3 kapime uonea matokeo

Mi nadhani hapo kabla ya kutumia kitunguu ni vizuri kujua ana presha ya aina gani.
 
kwanza niseme umefanya vema kuchanganya madoctor. Hii inakusaidia kuelewa vizuri ugonjwa wako pia madaktari nao hukosea. Kwa kawaida presha kuicontrol unaanza na kuchange lifestyle kama mazoezi na chakula. Ikishindikana unaongeza dawa ya kupunguzza maji kama lasix. Kwa pamoja maazoezi na hizi dawa zinaweza kupunguza kama 15mmhg. Kama haijafika 120mmhg unaongezewa beta blockers kama propanolol. Mi naona daktari 1a pili alikuwa sahihi maana dawa za kupunguza tu maji zisingeweza kukushusha hadi 120.
 
mriga vipi round za bed aziongezi hii mpwa??msaidiekwahiki pia

Hilo suala dawa yake ni mazoezi tu. Fanya mazoezi angalau nusu saa kila siku. Utaona mabadiliko mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…