Taa za barabarani kuanzia Stand ya Morocco hadi Biafra, Kinondoni, ambazo zilikuwa zimeharibika kwa muda na kusababisha giza hatarishi, sasa zimerekebishwa na zinafanya kazi vizuri.
Giza ambalo lilikuwa linahatarisha usalama wa watumiaji wa Stendi na barabara, ikiwemo watembea kwa miguu na magari yanayoingia na kutoka eneo lenye shughuli nyingi, limeondolewa.