SoC04 Tatizo la Traffic Police barabarani

SoC04 Tatizo la Traffic Police barabarani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Save NUNDU

New Member
Joined
May 2, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Tatizo la Traffic Police barabarani: wananchi tunacheleweshwa sana kwenye shughuli zetu tukiwa kwenye daladala kwa daladala hiyo moja kusimamishwa mara kadhaa na Traffic kwa trip hiyo hiyo moja. Kwanini zisitumike mbinu mbadala?

Viongozi wetu wanasafiri nchi za nje sana na wanaona nchi za wenzetu mfano Marekani huwezi kumuona Traffic Police barabarani, mimi niliishi Marekani na siku moja nilikuwa haraka nimechelewa kwenye appointment, nikiwa nimesimama kwenye traffic lights zikiwa nyekundu, niliangalia kushoto/kulia hakuna gari wala Police nikapita kwenye taa nyekundu!

Wiki mbili kabla, nilipokea barua kwenye mailbox ya nyumbani, kufungua ile barua nilikutana na picha ya gari langu likipita kwenye taa nyekundu tarehe ile ile niliopita pale na faini ya dola sabini imeandikwa humo na maelekezo ya kuilipa. Hizo ni mbinu za Serikali kufanya kwa kupunguza mapolisi barabarani.
 
Upvote 0
Mifumo ya kidijitali, ikisaidiana na akili bandia itatusaidia sana.

Nyongeza kwa Nundu: Kama uko na nia ya kushinda jazia nyama. Wanataka maneno kama buku hivi
 
Back
Top Bottom