Tatizo la Ujerumani na Uingereza

Messi Lionel

Senior Member
Joined
Jan 11, 2018
Posts
170
Reaction score
159
Pamoja na kusoma masomo ya Sayansi na Sanaa (Arts) katika maisha ya sekondary lakini nilipenda kweli masomo ya Sanaa kama History na Geography tangu primary mpaka sasa sijawahi kuachwa nyuma katika habari ya Historia..Jiografia hata Lugha lakini nakumbuka tuliambiwa Wakoloni wa Kijerumani waliondoka mapema sana baada tu ya kushindwa katika vita ya kwanza ya dunia(1914-1918),

Hivyo Mkoloni wa Kiingereza na Magavana wake wanne wakawaongoza mababu zetu tangu 1919 mpaka 1961 ambapo Mwalimu a.k.a Teacher akapewa uhuru alioudai kwa nguvu zote.

Kidogo nilichowahi kujifunza kutoka kwa hawa jamaa wawili wenye ngozi nyeupe ni kuwa,Mjerumani alifanikiwa kutuachia vitu vya mifumo ya kibabe na vilivyokuwa moja kwa moja(direct) wametuachia majengo magumu makubwa moja wapo ni makanisa ya Kilutheri ambapo mpaka nyimbo nyingi za kilutheri huwa zinafanana kabisa na Wimbo wa Taifa wa Ujerumani(alles alles uber alle) lakini pia majengo imara ya shule kama Iyunga Tech(levavo orculos).

Lakini Muingereza ndo alituathiri sana kwa kutuachia kila kitu kuanzia mifumo ya kiserikali,elimu,kupenda kutunza vya zamani(conservatism) lakini kibaya zaidi alichotuharibu ni kwenye suala la vyombo vya habari(media) ambapo jamaa hupenda sana kujitangaza hata kwa kitu kidogo kilichofanyika..

Mwaka jana nilijaribu kuiangalia michuano ya kombe la mabara(FIFA CONFEDERATIONS CUP) iliyoandaliwa na Urisi katika majiji yake kama Kazn,St.Petersburg,Moscow n.k na kuwachambua vizuri Wajerumani nikagundua kama ingewezekana Mjerumani atutawale mpaka 1961 kuna aina ya mfumo tungekuwa nao hata katika soka..Wajerumani wamekuwa bora sana katika idara mbalimbali katika Nchi yao..

Viwanda,Elimu,Teknolojia na hata katika Soka,tangu niwafahamu nikiwa na akili timamu mwanzoni mwa karne ya 21 mwaka 20O2 wakifika final..2006 mshindi wa 3..2008 final Euro..2010 mshindi wa 3 Kombe la Dunia kwa Mzee Madiba..2014 mabingwa world cup pale Maracana..unaona mtiririko wao wa kutunza ubora wao(maintanance of consistency) angalia vizazi vyao visivyopotea katika soka na vinatoa ubora uleule wa soka..

Tangu Ujerumani ya Michael Ballack,Odonkor,Stefan effenberg,Oliber Khan,Oliver Keuville..kikaja kizazi cha kina thorsten frinhs,Bastian Schweinsteiger,Cacau,jens Lehman,Hitzlperger,Trochowski,Miroslavklose, baada ya hapo kikaja kizazi cha mabingwa wa world cup.

kizazi cha Joachim Loew(Mesut Oezil,Sami Khedira,Tony Kroos,Bastian,Benedict Howedes,Lahm,Mats Hummels,Jerome Boateng,Marco Reus,Andre Schurrle,Jonas Hector,Mario Super Goetze,Manuel Neuer n.k
sasa wana kizazi cha kina Marc Andre Ter Stegen,Demirbay,Süle,Goretzka,Rudiger,Rudy,Werner n.k unagundua jamaa hawajawahi kuchemka kwenye kuunganisha vizazi vya soka...

Lakini kwa waingereza tazama wanavyokuwa na vizazi bora vya soka lakini wanajikita mno katika kucheza na media kuliko kutengeneza muunganiko wa timu(chemistry of the team)..kuna vizazi bora vilivyowahi kupita England kama kile cha kina Steven Gerrard,Super Frank 8 Lampard,Rio Ferdinand,John george Terry,Ashley Cole,Wayne Rooney,Michael Owen,Owen Hagreaves n.k lakini nje ya uwanja wanacheza mpira mnoo tatizo lilikuwa ni ndani ya uwanja.

Mpaka leo najiuliza tatizo ni mkoloni yupi hapa anatufikisha katika soka letu leo?

Lakini kama inawezekana twaweza kuiba hata kidogo vile vielementi vya mfumo wa soka la kijerumani...

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]...
 
Kwa mjerumani kila kitu bora bwana.kwanzia Soka hana mpinzani,, ukija kwenye utengenezaji wa magari ni chuma mtupu, ukija kwenye caterpillar machines aina zote kwanzia Grader, wil-loader, excavators, compactor na takataka kibao chuma mtupu, ukija kwenye mabarabara na madaraja wapo juu. Mjerumani ni rijali....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…