Tatizo la ujinga Tanzania bado ni kubwa

Tatizo la ujinga Tanzania bado ni kubwa

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
MJINGA NI NANI? NINI MAANA YA UJINGA?
#Kamusi (Dictionary) inatafasiri neno Ujinga (ignorance) kama ukosefu wa maarifa au taarifa juu ya jambo Fulani. Lack of knowledge or information.

#Kamusi (Dictionary) inaendelea kusema; Mjinga ni mtu anaeukataa au kuupuuza ukweli kwa makusudi. A person who deliberately ignore or disregard important information or FACTS.

#Mjinga ni mtu asie fahamu au asie na utambuzi wa jambo Fulani. The state of being unaware or even cognitive on a particular matter.
Kamusi ya TUKI imetafasiri neno Ujinga kama Hali ya kutojua kitu.

#Mark Twain anasema “#We never knew an #ignorant person yet but was prejudiced”. Bado hatujafanikiwa kumfahamu Mjinga maana TAFASIRI ILIYOPO YA NENO MJINGA HAIJITOSHELEZI (Prejudiced-insufficient, biased).

#Wajinga ni watu wanaopenda kubeza mambo ya maana. Watu wanaoleta masihara kwenye mambo ya msingi.

#Watu wanaofanya matendo ili kuwafanya wengine waonekane hawajui kitu au kupumbaza watu juu ya ukweli wa jambo Fulani.

#Wajinga ni watu wanaoweza kurubuniwa kirahisi kutokana na ukosefu wa maarifa muhimu(basic knowledge). Watu wanaoweza kuamini mambo bila kutafakari kwa kina.

JE, SISI KAMA NCHI TUNA TAFASIRI IPI JUU YA UJINGA?
#Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru 1961 na badae kuwa jamhuri 1962, Mwl Nyerere alitangaza vita dhidi ya maadui WAKUBWA watatu; Umaskini, Ujinga na Maradhi(Poverty, Ignorance and Disease). Azimio la Arusha 1967.

#Mwl Nyerere alisema; “Umaskini, #Ujinga na Magonjwa sio maadui wa Mzaha mzaha, ni maadui kweli kweli. Na mtu yeyote atakayekataa kushiriki katika mapambano dhidi ya vita hii au Atakayezuia jitidaha za jirani yake za kuishinda vita hii Atakuwa ametenda kosa kubwa la Usaliti kuliko Kosa la kumsaida adui aliyevamia Taifa letu kwa mtutu wa bunduki.

#Words of Mwl Nyerere “Poverty, #Ignorance and Disease” are not mock enemies, they are true enemies of our people. And anybody who refuse to take part in this war, or hinders the efforts of his neighbors, is guilty of helping a far more deadly foe than is he who helps an armed invader. (A very Real War, Popular Participation in Development in Tanzania Duriing the 1950&1960, by Michael Jennings)-International Journal of African Historical Studies Vol.40, no 1(2007)

#Kwa mantiki hii ya Mwl Nyerere, Ujinga ni adui mkubwa sana, mwenye nguvu na ujanja mwingi.
#Katika kipindi cha miaka #58 ya Uhuru, Taifa la Tanzania, limezalisha #wajinga wa kisasa(Modern ignorants). #Hawa wanajua kusoma na kuandika mpaka #kingereza, na wengi wao wamepata shahada za Vyuo Vikuu. Hawa ni wajinga hatari kuliko wale wasiojua kusoma na kuandika.

#Ile tafasiri yetu ya mwaka 1961, Kwamba Mjinga ni mtu asiejjua kusoma na kuandika haikubeba tafasiri sahihi. Mimi naungana na Mark Twain, kwamba Bado hatujafanikiwa kuwa na tafasiri inayojitosheleza juu ya Ujinga. Na kwa sababu hiyo, Tunawezaje kushinda Vita kama Hatumfahamu adui?

#Ndugu zangu, UJINGA UMEANGAMIZA MATAIFA MENGI YA AFRIKA NA MASHARIKI YA KATI. Plz Tuamke, TUTAFAKARI NA KUTAFASIRI UPYA NENO HILI. Leo hii, Mission nyingi za Mataifa yenye Nguvu zimefanikiwa kutokana na Ujinga wa WAAFRIKA WENYEWE.

#Tutoe wito kwa #midahalo na makongamano ya Kitaifa ili Tuutafasiri Ujinga kwa namna pana na kutengeneza framework ya kuukabili.
 
Ujinga ni kusingizia mabeberu na upinzani kwamba wanatukwamisha. Wakati upinzani umekuja juzi tu.
 
Back
Top Bottom