Habari, Ndugu Mteja.Kuna tatizo kubwa la umeme wilaya ya chunya umeme ni mdogo sana. Hili tatizo limekaa muda sasa zaidi ya miezi miwili.
Mahitaji ya umeme kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za madini ni makubwa mno. Kukatika kwa umeme eneo hili kunaleta hasara kubwa sana kwa watumiaji.
0782510235 Meneja Tanesco Chunya!Habari, Ndugu Mteja.
Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja.
Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu. Kutokana na changamoto ya muda iliyojitokeza kwenye akaunti yetu, ujumbe wako ulitufikia kwa kuchelewa. Hata hivyo, kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.
Tafadhali, tunaomba kutufahamisha kama changamoto uliyoiwasilisha bado inaendelea au tayari imetatuliwa. Endapo bado unaikabili, tafadhali tujulishe ili tuweze kuifuatilia na kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi kwa haraka.
Asante sana kwa uvumilivu na ushirikiano wako. Karibu sana. ^CM
Asante, ndugu mteja.0782510235 Meneja Tanesco Chunya!
Muulizeni atawajibu, hali halisi ilivyo,huko Chunya!
Hali ni mbaya ,Mbaya ,mbaya kabisa.
Low voltage mchana hakuna umeme wa kutosha, usiku pia na siku za Alhamis na Jumamosi hakunaga umeme kabisa kwa kila wiki.
Hili ni janga la Taifa
Habari, Ndugu Mteja.Kuna tatizo kubwa la umeme wilaya ya chunya umeme ni mdogo sana. Hili tatizo limekaa muda sasa zaidi ya miezi miwili.
Mahitaji ya umeme kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za madini ni makubwa mno. Kukatika kwa umeme eneo hili kunaleta hasara kubwa sana kwa watumiaji.
Habari, Ndugu Mteja.Tanesco uwajibikaji wilaya ya Chunya ni hafifu.. Umeme umekua ni changamoto hasa kwa biashara hii ya madini.. Umeme umekua zaidi ya kero tunaingia gharama kubwa kutumia mafuta na mnaelewa hali ya bei ya mafuta ilivo.. Kwa kweli mnatia hasara na mnakwaza tunakaa siku nzima umeme hakuna na ukirudi ni masaaa kadhaa umekatika tena na hii inaenda wiki nzima.. This is too much
Asante kwa taarifa nzuri!Habari, Wateja Wetu.
Tunapenda kutoa mrejesho kuhusu changamoto ya umeme kuwa mdogo (low voltage) inayowakabili baadhi ya wateja wetu katika Wilaya ya Chunya na wilaya ya Mkwajuni.
Tafadhali fahamu kuwa Serikali kupitia TANESCO inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto hii. Leo Septemba 11, 2026, mkataba wa ujenzi wa miundombinu muhimu ya umeme umesainiwa Wilayani Mkwajuni, hatua ambayo inalenga kuongeza upatikanaji wa umeme kwenye wilaya hizo.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 (220kV) kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, Wilaya ya Mkwajuni, yenye urefu wa takribani kilomita 122, kwa thamani ya TSh bilioni 109. Aidha, mradi unahusisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme chenye uwezo wa 100MVA, sawa na takribani MW 80.
Mradi huu unatarajiwa kuleta kutatua changamoto yote ya upatikanaji wa umeme kwa wateja wote.
Hivyo, tunaomba muendelee kuwa na uvumilivu wakati utekelezaji wake unaendelea.
Tunawashukuru kwa ushirikiano na uvumilivu wenu.
Asante! ^HN
Habari, Ndugu Mteja.Asante kwa taarifa nzuri!
Ninaomba kuuliza, kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, Wilaya ya Mkwajuni, yenye urefu wa takribani kilomita 122, hii line itapitia chunya mjini, Matundasi hadi Makongorosi? Ua itapitia wapi?