Tatizo la utundu uliopitiliza na kukosa utulivu kwa watoto

Joined
Nov 3, 2014
Posts
38
Reaction score
10
KITAALAM TATIZO HILI LINAITWA (ATTENTION DEFICIT HYPERACTIVITY DISORDER (ADHD)
Watoto wenye tatizo hili ni wale ambao wana shida ya kukosa utulivu, kukurupuka na kua na utundu uliopitiliza
Dalili zinazoashiria Utundu uliopitiliza (hyperactivity symptoms)ni kama
• muda wote anahangaika/kuzunguka zunguka
• anasimama hata wakati ambapo anatakiwa kua amekaa
• muda mwingi ana kimbia kimbia au kupanda juu hovyo isivyotakiwa.
• Anaongea kupita kiasi
• Hawezi kutulia au kucheza kimya
• Muda wote ni kama anaongozwa na motor… ni…..shi shiddah
• Anaweza pia kua na hasira

Dalili za kukosa utuli
vu (inattention symptoms)ni kama zifuatazo
• Hayupo makini katika vitu vidogodogo.
• Anafanya makoza ya kizembe
• Hawezi kutuliza akili katika jambo au kitu kimoja.
• Anakua kama hakusikilizi unapoongea nae
• Ana shida ya kukumbuka vitu anapopewa maelekezo
• Anashindwa kupangilia mambo au kuunda kitu
• Anachoshwa na kazi kirahisi hata kabla ya kuimaliza
• Anapoteza vitu mara kwa mara mfano kalamu, penseli vitabu N.

Dalili za Kukurupuka (Impulsivity symptoms) ni kama
Anazunguka muda wote, hatulii na anaweza kua anaropoka hovyo, hasikilizi maelekezo.yawezekana ikamsababishia ajali au kuumia mara kwa mara. Makovu mengi yatokanayo na ajali.

Matibabu ya matatizo ya kitabia kwa watoto
Watoto bila kutibiwa matatizo ya kitabia wnaweza kukua na kuwa watu wazima wasioweza kufanya kazi. Kwa ujumla, KUTAFUTA MATIBABU mapema, kuna uwezekano wa kuwepo matokeo mazuri.

Matibabu ni kawaida yapo ya aina nyingi na inategemea ugonjwa na mambo yanayo changia hilo tatizo la tabia, lakini ni pamoja na:

Elimu kwa wazazi - kwa mfano, kufundisha wazazi jinsi ya kuwasiliana na na kusimamia watoto wao. Jinsi ya kumdhibiti na jinsi ya kucontrol tabia zisizofaa

Tiba kwa familia - familia nzima inasaidiwa kuboresha mawasiliano na mbinu za kutatua matatizo.

Tiba ya Utambuzi wa kitabia – lengo hapa ni kumsaidia mtoto kudhibiti mawazo, hasira, na tabia zisizokubalika. hii hufanywa na wataalam wa saikolojia na malezi ya watoto

Mafunzo ya Jamii – kumfundisha mtoto stadi muhimu za kijamii, kama vile jinsi ya kuwa na mazungumzo au kucheza kwa kushirikiana na watu wengine.

Usimamizi na jinsi yakutatua wa hasira - mtoto hufundishwa jinsi ya kutambua dalili za hasira na kupewa mbinu mbalimbali ya kukabiliana na dalili hizo. Motto pia anasaidiwa kupunguza matatizo ya hasira yao na tabia ya fujo na kutotulia. Mbinu ya kupumzika na ujuzi wa usimamizi wa hisia pia hufundishwa.

Msaada kwa ajili ya matatizo yanayohusiana - kwa mfano, mtoto na shida ya kusoma , kuongea, kifafa, n.k watafaidika kutokana na msaada wa kitaalamu kutibu matatizo hayo.

Dawa – zipo dawa ambazo husaidia husaidia kudhibiti msukumo wa tabia na hali ya kutotulia

Wapi pakupata msaada

daktari wa watoto, psychologist wa watoto au mtaalam wa magonjwa ya akili ya watoto)
 
Sasa Dawa yao nini.., Kiboko sio!
kiboko huzidisha tatizo na kusababisha matatizo mengine kama wizi n.k

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…