SoC02 Tatizo la vijana kushindwa kujiajiri

SoC02 Tatizo la vijana kushindwa kujiajiri

Stories of Change - 2022 Competition

Elisha Kigahe

Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
5
Reaction score
4
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kukosa ajira. Makala hii, itaangazia changamoto zinazo wakabili vijana katika sekta ya ajira binafsi.

Kutokana na wingi wa vijana wanaohitimu vyuo vya kati na vyuo vikuu, suala la ajira limekuwa tatizo sugu hapa Tanzania.

Mifumo yetu ya elimu inawaandaa vijana kuajirika katika sekta za umma na sekta binafsi. Hivyo, kutokana na uwingi wa wahitimu wa vyuo, mahitaji ya soko yamezidiwa na Kasi ya wahitimu. Hii imepelekea suala la ajira rasmi kukumbwa na bumbuwazi.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na msukumo mkubwa wa viongozi na wanazuoni mbalimbali wa kutaka vijana wajikite katika kujiajiri au ajira binafsi.

Ukweli ni kwamba ajira binafsi zinakumbwa na changamoto nyingi. Mazingira yake Bado hayaruhusu urahisi wa kufanikisha adhima hiyo.

Makala hii inaangazia baadhi ya changamoto ambazo serikali na wadau wengine wanapaswa kuzitazama kabla ya kushikia mabango suala la kujiajiri kwa vijana.

CHANGAMOTO ZA AJIRA BINAFSI KWA VIJANA.


1. MFUMO WA ELIMU


Hapa tunaangalia madhaifu yaliyopo katika mfumo wetu wa elimu. Mfumo wa elimu yetu ni ule ambao umerithishwa kutoka kwa wakoloni. Ikumbukwe kuwa lengo kuu la elimu ya mkoloni ilikuwa kuwaandaa watu watakao tumika kwenye makampuni yao. Wakoloni walitoa elimu kwa baadhi yao ili waweze kuajiriwa Kama vibaraka wao. Mfano makalani wa mashamba ya chai enzi za mkoloni. Kwa mfumo huu ni ngumu kumuandaa kijana kujiajiri.

Kuna udhaifu mwingi katika mfumo wetu wa elimu, kiasi kwamba inakosa tija kwa vijana wetu.


MADHAIFU YA MFUMO WA ELIMU YETU

A. Kijana anatumia muda mrefu sana kutimiza malengo yake ya kielimu. Inamchukua muda wa zaidi ya 16 kutafuta elimu. Hii inawafanya vijana kukosa muda wa kujitanua kulingana na mahitaji ya kimazingira. Muda wote huu anakuwa ametingwa na masomo sambamba na mitihani.

B. Elimu yetu ina mawanda mapana ya taarifa ambazo mwanafunzi anatakiwa kuyabeba. Hii inapelekea vijana kukosa umahili wa eneo moja. Kwa mujibu wa wanafalsafa mbalimbali, ni ngumu Sana kuwa mahili kwenye kitu zaidi ya kimoja. Mfano, kijana wa kidato Cha nne anabeba masomo zaidi ya 9 ambayo yamejiegemeza katika sanaa, sayansi na biashara. Hii inamnyima mwanafunzi uwezo wa kuwa mahiri.

C. Elimu yetu ni dhahania kuliko vitendo. Taarifa nyingi zinazobebwa katika masomo yetu ni dhana za kuvikilika. Hivyo, inakuwa ngumu kwa kijana kutumia elimu yake kujiajiri kulingana na mazingira yetu.

D. Elimu yetu haiendani na uhalisia wa mazingira yetu na wakati wetu. Kuna baadhi ya mafunzo hayaendani kabisa na mazingira yetu ya Sasa. Hii inafanga vijana kushindwa kutumia elimu Yao katika kupambana na maisha.

Kwa ujumla, mfumo wa elimu yetu haimuwezeshi kijana kujiajiri. Tunahitaji maboresho makubwa katika mitaala ya elimu ili kukidhi haja ya mazingira ya Sasa.

Maboresho tunayoweza kufanya kwenye mfumo wetu wa elimu ni pamoja na muda wa kuanza na kumaliza shule upunguzwe, mawanda ya masomo yapunguzwe. Mwanafunzi aanza kuchagua taasusi au mkondo kuanzia shule ya msingi Hadi elimu ya juu. Hii itasaidia kuongeza tija katika sekta ya ajira binafsi.


2. KUKOSEKANA KWA MTAJI

Sababu nyingine inayoongeza ugumu kwa vijana wengi kujiajiri ni kukosekana kwa mitaji.

Ili uweze kuanzisha au kuendesha biashara yeyote unahitaji mtaji. Vijana wengi wanatokea katika familia duni kiuchumi. Hivyo wanashindwa kupata msaada kutoka wa wajumbe wa familia zao.

Licha ya jitihada za serikali kujaribu kutatua tatizo hili kwa kutenga 10% ya mapato yote ya halmashauri kwa mwaka, Bado uhitaji ni mkubwa kuliko kilichopo. Bado serikali haiwezi kuwafikia vijana wote wenye nia ya kujiajiri.

Zipo baadhi ya taasisi za fedha zinazotoa fedha ambazo zinaweza kutumika Kama mtaji. Masharti yake yamekuwa magumu kufikiwa na vijana wengi. Mfano, wanahitaji uje na dhamana ya mali isiyo hamishika Kama nyumba. Inakuwa ngumu kwa vijana wengi kukidhi kigezo hiki.

Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau mbalimbali Bado suala la mtaji limekuwa changamoto kubwa.

3. KUKOSEKANA KWA UBUNIFU MIONGONI MWA VIJANA

Vijana wengi wanashindwa kubuni au kuibua biashara mpya zitakazo tatua matatizo katika jamii. Hii inawafanya wafanye biashara kwa historia za watu wengine.

Wanapenda kuiga biashara za watu kwa kusikia faida zake. Hii inapelekea kushindwa kumudu changamoto za biashara hiyo.


4. UTITILI WA KODI NA TOZO

Kumekuwa na Kodi, ushuru na tozo nyingi ambazo zinapunguza tija katika biashara za vijana. Ni wajibu wa Kila Mtanzania kulipa Kodi kwa maendeleo ya taifa letu. Lakini, zikizidi inapelekea kuanguka kwa biashara nyingi. Mfano, unasafilisha mazao ya misitu unatakiwa kulipa (kibali cha ofisi ya misitu, ushuru wa halmashauri, ushuru wa usafilishaji, Kodi ya serikali 5%) Hii inapelekea biashara nyingi kushindwa kujiendesha.


5. UVIVU NA TABIA YA KUTOPENDA KAZI

Baadhi ya vijana ni wavivu, hawapendi kufanya Kazi. Wanakesha kwenye mitandao ya kijamii. Vijana wengi hawajitambui


HITIMISHO

Kwa kuhitimisha, sekta ya ajira binafsi ndio sehemu pekee ambayo itakwamua taifa kutoka katika janga la vijana wengi kukosa ajira.

Inapaswa kutengenezewa mazingira wezeshi Kama vile mitaji ya Hali na mali, mikopo rahisi, elimu ya biashara, sera zinazotabilika na kadharika.

Asante kwa muda wako ulioutoa kwaajili ya kuisoma makala hii.

IMEANDALIWA NA:
ELISHA KIGAHE
0757366084
 
Upvote 7
Nakupigia kura kwasabbu umekuwa muugwana kwa kutukumbuka na kutushukuru kupitia andiko lako,umejitahidi kugusa baadhi ya maeneo muhimu yanayokwamisha kijana kujiajiri hasa ukosefu wa ubunifu kutatua changamoto zinazomzunguka kijana,ukosefu wa umahiri wa mapema katika fani ingawa wengi hudharau huu ujuzi nakuuona ni kwa wale walishindwa kuendelea na masomo,hapa ni vyuo vya ufundi
Kuhusu mtaji ni kweli ni tatizo Ila hata ungekuwa wewe nadhani Kama utampatia mtu pesa ya andiko lake la ufugaji kuku wa kisasa 1000 wakati hata kuku 100 ameshindwa kuonyesha amefugia wapi nawe utakuwa umekosea.
Yote kwa yote wahitimu wa elimu yeyote nao wanapaswa wajitambue wawapo vyuoni kuna maisha baada ya kumaliza elimu zao wanayopaswa kuja kukabiliana nayo wamalizapo elimu hizo wasifumbe macho kutokuona yanayojiri nje ya vyuo kwa kuamini watakapomaliza wakiwa na ufaulu mzuri watapata ajira,vyuoni kuna uwezekano mwingi w kupata taarifa sahihi,kujenga networks ambazo zinaweza kuja kukusaidia baadae.ila ndio hivyo tena ni wepesi wa kulaumu tulipo angukia na kushindwa kukiona kisiki kilichotuangusha.
Tuishi katika uhalisia hasa tuachane na hizi ndoto za mafanikio utayapata kwa kwenda kuajiriwa,unadhani anaekuajiri nae Kama ha kutoka nje ya box la kuajiriwa si nae asingekutengenezea wewe ajira,
Ajiriwa ilikupata ujuzi,na mtaji ukishavipata usiwe mvivu na mwoga toka nenda katengeneze mazingira nawe uajiri,na kwa watakaokosa kuajiriwa wasikate tamaa waanzie chini kujitengenezea ajira kwa mazingira waliyonayo,mfano Kama ni mtoto wa kijijini au mtoto wa masikini anaweza kuangalia fursa zinazomzunguka akaanza taratibu akitafuta mtaji na maarifa mbadala wa kuboresha kama ni kilimo,ufugaji,biashara ambavyo kwavyo wazazi wake walitumia kumsaidia mpaka akafika hapo alipo.
Kama ni wa mjini nae pia anaweza kujichanganya kupata ujuzi wa ziada wenye kumsaidia kupata kipato,mfano ufundi rangi,udereva bodaboda,bajaji mpaka magari makubwa then aka vitumia wakati anapambania kombe lake,pia kama wazazi wake nao walijiongeza waawa hata na kamradi ka genge ambalo ndilo lililomsomesha akafika hapo alipo anaweza tumia pia Kama chanzo cha maarifa ambalo anaweza kuboresha hali yake nakukuZa mtaji,Mimi hupenda sana wafanyamiashara wa matunda kwanihuwasogeza wengi mbolea Kama wanakuwa makini
 
Back
Top Bottom