Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

MyTanzania

Senior Member
Joined
Sep 9, 2008
Posts
106
Reaction score
8

Ndugu zangu ndani ya JF habari zenu.

Mimi nina matatizo ya vipele mwisho wa nywele za kichwani upande wa kisogoni ambavyo vinatokana na kunyoa.

Nimepata ushauri kwa madaktari mbalimbali juu ya dawa za kutumia bila mafanikio.Kama kuna mtu anajua ni namna gani naweza kutibu na pia kuzuia visitokee tena naomba tuwasiliane humu JF.

Nimeona watu wengi hivi karibuni wamekuwa na hali hiyo ambapo baadhi inapelekea kuota nyama kubwa baadaye. Naomba anayejua asaidie,maana najua watu wengi wanahangaika sana kuutibu ugonjwa huo sasa.

Nitashukuru kwa mtu yeyote aliye tayari kutoa msaada wa ushauri na hata kama kuna dawa aiandike humu niitafute.
Asante.
WENGINE WENYE KUHITAJI UFUMBUZI WA TATIZO HILI



FAHAMU TATIZO LA ACNE KELOIDALIS NUCHAE

Acne Keloidalis Nuchae ni nini?
Licha ya jina, acne keloidalis nuchae sio aina ya chunusi. Ni aina ya folliculitis, na dalili ambazo zinafanana na chunusi. Kwa kawaida huwa kama upele karibu na sehemu ya nywele upande wa nyuma wa shingo. Mwishowe haya huwa makovu na nywele zinzozunguka eneo hilo zinaweza kuondoka.

Tatizo hili linaweza kuwa lisizofurahisha, kukera na lenye kuleta maumivu na msongo wa mawazo. Wagonjwa wengi wa tatizo hili hupoteza kujiamini.

Folliculitis kwa upana inahusu kuvimba au kuambukizwa kwa follicle, yaani vishimo vya nywele. Folliculitis ni ugonjwa wa kawaida wa ngozi ambao unaweza kutokea mahali popote kwenye mwili ambapo nywele hukua.

Visababishi vya Acne Keloidalis Nuchae
Sababu haswa haijulikani. Walakini, kuna nadharia kadhaa za kuelezea hali hiyo, pamoja na:
  • Kunyoa au kukatia nywele chini sana
  • Kofia na mavazi
  • Homoni
  • Reaction ya kinga mwili
  • Masuala yahusuyo vinasaba
Kunyoa au kukatia nywele chini sana. Kuumia kwa ngozi kunaweza kutokea kutokana na kunyoa kwa karibu au kukata nywele na wembe, ambayo inaweza kuharibu ngozi ya nywele na kusababisha kuvimba.

Kofia na mavazi. Helmet au collars zilizovaliwa karibu na shingo zinaweza kuvuta kwenye nywele na kusababisha msuguano. Mvutano huu unaweza kuzidishwa na joto au jasho.

Homoni. AKN hutokea karibu kwa wanaume wazima, na kupendekeza kwamba androjeni zinaweza kuchukua jukumu moja kwa moja au kwa njia isiyo sawa.

Reaction ya kinga mwili. Antijeni ndani ya follicles ya nywele huvutia seli za uchochezi, na kusababisha uharibifu wa ukuta wa follicular na, mwishowe, upotezaji wa nywele (shida ya alopecia).

Masuala yahusuyo vinasaba

Nani yuko hatarini?

AKN huathiri kati ya 0.45% na 9% ya idadi ya watu. Inasemekana huathiri zaidi wanaume wenye ngozi nyeusi, haswa wale wa asili ya Kiafrika, ingawa inaweza pia kuwaathiri wenye ngozi nyeupe. Hali hii huanza baada ya ujana na ni nadra sana baada ya miaka 55.

Wanaume walio na nywele ngumu (kinky) wanahusika hasa na hili. Wakati hakuna uhusiano wa moja kwa moja, inadhaniwa kuwa hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya kukata nywele na ni trauma inayosababishwa na wembe wa umeme. Kupindika kwa follicle ya nywele kwenye ngozi inaweza pia kuwa sababu.

Tatizo hili lipoje kwa wanawake?
AKN haipatikani sana kwa wanawake, na wanaume wakiwa na uwezekano wa zaidi ya mara 20 kupata hali hiyo. Hii inaipa nguvu nadharia kuhusu mazoea ya kukata nywele, kwa kuwa wanawake wana uwezo mdogo wa kunyoa nyuma ya shingo. Pia inaimarisha nadharia ya kuwa homoni zinaweza kuchangia katika hali hiyo.

Matibabu kwa dawa za Over the Counter
Makundi haya ya dawa zinaweza kutumika kutibu tatizo hili.
  • Antimicrobial cleansers
  • Triamcinolone cream
  • Topical steroids
  • Oral antibiotics
  • Oral isotretinoin
Ufanisi wa dawa kwa AKN hutofautiana kati ya watu.

Endapo dawa za Over The Counter zikishindwa kufanya kazi, wagonjwa wanaweza kuzingatia matibabu yafuatayo:
  • Matibabu ya laser
  • Matibabu ya upasuaji
  • Radiotherapy
Unachoweza kufanya ili kuizuia AKN
Wakati matibabu ya AKN yanaweza kuwa magumu, kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya dalili zinazoendelea. Ikiwa tayari unasumbuliwa na hali hiyo, mazoea haya ya maisha yanaweza pia kuzuia dalili kuwa mbaya.
  • Epuka kunyoa au kukata nywele fupi sana ambavyo inaweza kuharibu nerve follicle.
  • Epuka kuvaa mavazi, kofia au helmeti ambazo hutambaa nyuma ya shingo.
  • Epuka kutumia bidhaa za nywele kama hairsprays, gels au pomades, ambazo zinaweza kuingilia ukuaji wa nywele.
  • Hakikisha shingo yako ni safi na kavu wakati wote
  • Kuwa makini wakati wa kusafisha ngozi nyuma ya shingo, kwani kusugua kwa bidii kunaweza kusababisha kuwasha.

MICHANGO YA WADAU
 
Pole sana ndugu kwa tatizo hilo linalokusumbua. Napenda kuuliza je ukiacha bila kunyoa muda mrefu vipele hivyo bado vinajitokeza, au ni pale tu unaponyoa?
 
Wembe zinaleta vipele jaribu kutumia mashine ya kwako peke yako.
 
Wembe zinaleta vipele jaribu kutumia mashine ya kwako peke yako.

Kweli kabisa, miye situmii nyembe hata kidogo, na kwa ma barbers ndiyo kabisa usipoangalia unaweza jikuta unarudi na magonjwa ya kila aina ya ngozi.

Naona hajapata chance ya kujibu swali langu nililomuuliza hapo mwanzo.

Nilitaka ku-suggest ajaribu pia njia nyingine abstract; afuge rasta. Huwezi jua, kunaweza kumsaidia.
 
Nashukuru Steve D na YO Yo kwa kuonyesha concern.Nisiponyoa muda mrefu haviendelei kuota,ila sasa shughuli ninayofanya hainiruhusu kufuga rasta,ningekuwa nina shughuli yangu mwenyewe ningefuga,kwani hili tatizo limekuwa kero sana kwangu.

Nimenunua mashine yangu mwenyewe lakini nadhani tatizo liko pale pale kwenye nyembe.Ila kuna mtu kanishauri nitumie mkasi kunyoa lakini sijapata mtaalamu wa hiyo nyenzo maana vinyozi wengi siku hizi wamesahau kutumia kifaa hicho ambacho tulitumia zamani.

Asanteni sana,bado nasubiri ushauri zaidi.
 
MyTanzania, samahani natoka nje kidogo ya mada, kwanini lakini rasta hawaruhusu sehemu unayofanyia kazi?!
 
Pole sana kwa tatizo la vipele. Jaribu kutumia maji ya moto sana kila baada ya kunyoa kujikanda kwenye hizo sehemu. Nilipata huo ushauri toka kwa rafiki yangu nikaujaribu kwa mtu ukakubali.

Hata kama unapata hilo tatizo ukinyoa ndevu, jaribu kutumia maji ya moto sana kila unaponyoa unajikanda na tatizo litakwisha. Ukifanikiwa saidia na wengine.
 
My Tanzania,

Tatizo unalozungumzia limeshawakumba watu wengi na hasa wale wanaopenda kunyoa nywele zote kichwani (kipara). Kitu ninachoweza kukushauri unapokwenda kunyoa salon punguza nywele kwa kiasi cha kutumia kitana kidogo kabisa ambacho nadhani ndio size ya mwisho kuchania.

Pia mwambie kinyozi kuwa asikuchonge sehemu ya nyuma ya kichwa na hasa hayo maeneo zinapoishia nywele kuna uwezekano mkubwa ukaepukana na hili tatizo. Kuna siku nilihama salon baada ya kukuta mtu ananyolewa na ana vipele mwisho wa nywele then kinyozi akapitisha mashine pale ni damu kwa kweli nilistuka sana na hapo nami nikapata wazo la kununua mashine yangu mwenyewe.
 
Steve D
Tatizo la mabepari hilo inabidi tukubali tu kwakuwa tunataka cha uvunguni otherwise tunatakiwa kuwa watu huru.

MUHA
Nashukuru pia kwa ushauri wako,leo ninaanza kuutumia na ukinisaidia nitasaidia wengine pia.Asante saaaaaaaaana

KIPANGA
Nashukuru kwa ushauri wako,nitaanza kunyoa nabakisha nywele kwa kutumia mashine yangu mwenyewe.
Asanteni sana nikifanikiwa nitalirudisha humu JF ili wengine nao wafaidike na ushauri mlionipa.
 
Kuna jiwe linaitwa shabu kama chumvi ya mawe hili linaondoa tatizo kabisa, unachovya kwenye maji na kupaka baada ya kunyoa. Saloon za wahindi mjini zote hutumia.
 
Acha kukwangua ukienda saluni kunyoa. Wewe una alergy na metal
 
Habari wakuu,

Kuna tatizo la kutoka na vijiuvimbe vidogo vidogo kama vipele sehemu ya nyuma ya kichwa karibu na shingo. Kuna yeyote anayejua chanzo chake na dawa ya tatizo hilo? Naomba msaada wenu.
 
Mkuu tafuta dawa inaitwa candiderm ni ya kupaka inauzwa tshs 2500 mpaka alfu tatu kuna jamaa yangu imemtibu miaka km sita iliyopita yaani kalitunza hilo box lake mpaka leo jinsi vilivyomtesa
 
mkuu tafuta dawa inaitwa candiderm ni ya kupaka inauzwa tshs 2500 mpaka alfu tatu kuna jamaa yangu imemtibu miaka km sita iliyopita yaani kalitunza hilo box lake mpaka leo jinsi vilivyomtesa

Ahsante sana mkuu, ngoja niijaribu hii. Vimenisumbua sana huwa vinapotea then vinarudi tena!!
 
Nenda kwa wataalam wakushauri, sisemi kama ushauri wa hapo juu mbaya ila vyako vinaweza kuwa tofauti. Unaweza uka under/over dose.
 
Mkuu kuna sababu nyingine ambayo haihitaji dawa yeyote ile. Mimi ilianza kunitokea hali kama hiyo. Niliambiwa ni mafuta huwa yanajirundika na kuziba matundu ya hewa. Hivyo dawa wakati wa kuoga hakikisha unasugua eneo hilo kwa kitaulo kidogo.

Hakikisha unafanya hiyo kila siku utaona mabadiliko. Ukiona vinaendela basi ujue ni tatizo lingine tuu. Ila kwangu haikuchukua hata wiki mbili vilikauka na kupotea kabisa. Kwa hiyo nimejijengea tabia ya nikioga lazima nisugue maeneo hayo na kijitaulo.
 
Wadau kuna hivi vipele sugu nyuma ya kisogo,,vinasumbua sana kwa mda sasa,,ipi dawa yake na wapi naweza kutibiwa?
 
Wakuu naombeni msaada, nina sumbuliwa sana na vipele vya chini ya kisogo, yaani vinaniwasha mpaka nakosa raha. Mwanzoni nilifikiri vinatokea kwa sababu ya kushare mashine za kunyolea salon na nikaamua kununua mashine yangu lakini vipele bado havijaisha.

Naombeni ushauri wakuu nitumie dawa gani ili niweze kuondokana na vijipele hivi? Maana siwezi acha kunyoa nywele moja kwa moja.

Natanguliza shukrani.
 
Kwa ushauri wangu,ningekushauri uwe unanyoa katika saloon moja au mbili yaani usiwe unanyoa katika saloon nyingi sana. Na ili vipungue kuna sabuni inaitwa ''Kopacabana black spot soap'' ni nzuri. Inauzwa katika maduka ya cosmetics(vipodozi).

Ni sabuni nzuri unatakiwa uwe unaitumia kunawa nayo kila asubuhi na jioni. Jambo jingine muhimu ni kuacha kuchonga nyuma.
Ila kwa ushauri zaidi waone madaktari bingwa wa ngozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…