Tatizo la Wanawake Kupata Maumivu Wakati na Baada ya Kujamiiana: Fahamu Sababu na Suluhisho la Tatizo

Nimekuwa Napata kesi nyingi sana kutoka kwa akina mama hasa wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea wakihitaji msaada kwenye ndoa zao, maana hawafurahii tendo la ndoa kama vile inavotakiwa. Tatizo linazidi kuongezeka kwa kasi na wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hili hivo inakuwa vigumu kulitibu. Leo tutaongelea chanzo cha tatizo na jinsi ya kuepuka na kulitibu ili uendelee kufurahia unyumba. Wanawake hawakuumbiwa matatizo ya kiafya.

SABABU ZA KUPATA MAUMIVU WKATI WA TENDO LA NDOA
1. KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida Albicans) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.

2. Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.

3. Kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi (Uterus). Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini `fibroid` ni maarufu Zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hu kua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.

4. Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana sana eneo hilo, tatizo ambalo hujulikana kitaalam kama Hyrosalpinx.

Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya.

Kutoshika mimba kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.

Kumbuka matatizo ya uzazi unayokutana nayo kama maumivu makali kipindi cha hedhi, ugumba, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, mpangilio mbaya wa hedhi, uzito mkubwa na kitambi siyo kitu ulichoumbiwa, bali ni matokeo ya Maisha unayoishi .kwa kifupi matatizo yote haya chanzo chake kikubwa ni kuvurugika kwa homoni za kike au hormonal imbalance. Matatizo haya siyo kwamba ni mabadiliko ya vinasaba kutokana na umri, ila ni matokeo ya mpangilio mbovu wa vichocheo ama homoni zako na hasa homoni za uzazi. Hivo utakubaliana nami kwamba wanawake hawajaumbiwa kupata shida hizi zote hata kama umri wako umeenda, unahitaji kuendelea kufurahia tendo la ndoa. Sawazisha mpangilio wako homoni zako na matatizo yote haya utakuwa umeyakimbiza.

DALILI ZIFUATAZO ZINAASHIRIA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZAKO
Hivo unatakiwa kutumia dalili hizi kujifanyia uchambuzi wewe mwenyewe bila hata kufanya vipimo hospitali tayari utagundua kuwa una tatizo kwenye vichocheo ama homoni zako

1. Uzito kupungua ama kuongezeka bila mpangilio

2. Tumbo kujaa gesi na kuhisi umeshiba mda mwingi

3. Maumivu ya kichwa na kujuskia haupo kwenye mood nzuri

4. Kupata msongo wa mawazo mara kwa mara

5. Ugumba ama kutoshika mimba kwa kipindi kirefu

6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama kupata maumivu makali wakati wat endo la ndoa

7. Kuhisi mwili umechoka mara kwa mara

8. Kuota ndevu na nywele kifuani

9. Kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu

10. Kutokwa jasho jingi usiku na

11. Ngozi kukakamaa

12. Kukosa usingizi

13. Uvimbe kwenye mfuko wa mimba

Baada ya kujifanyiaupembuzi juu ya tatizo lako sasa tuangalie nini cha kufanya ili uweze kutibu dalili hizi kuanzia leo ukiwa nyumbani kwako.

ANZIA JIKONI KWAKO (LISHE /CHAKULA NI SEHEMU YA KWANZA YA KUREKEBISHA)
Nataka nikwabie mpenzi msomaji na unayefatilia Makala hizi kwa makini, kwamba vitu tunavyoweka tumboni vianchangia karibu 80% ya kuvurugika kwa mpangilio wa homoni zako. Unatakiwa kuwa mvumilivu maana kusawazisha homoni ni kitu endelevu na kinachukua kuda kutokana na kwamba unajenga tabia mpya kwenye mwili wako. Hivo hatua ya kwanza katika kupangilia lishe na mlo wako

Endelea kusoma zaidi kutia linki hapa chini

Chanzo: Mkumbo Health


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo vipi,

Juzi kuna msichana nimelala nae then baada ya tendo la ndoa akaniambia anasikia maumivu chini ya kitovu, dah! Mimi nikawa nampa pole nikamuuliza inaweza ikawa inasasabishwa na nini akatulia na kupotezea.

Sasa leo nimemueleza rafiki yangu mmoja, eti akaniambia ndio mimba imenasa.

Je, nini ukweli wake wadau?
 
tendo la ndoo ndio nini???????
 
Punguzeni kuzin wakat huu wa mvua, ninyi ndo mnaosababisha watoto vilaza
 
Mwanamke asipofika kileleni tumbo hadi mgongo sehemu hizo ziauma . proven scientifically . kama anakupenda atakuambia ,lla kama siku hiyo ukimuuliza alifika kileleni atasema hajui. Ila wanawake wengi wata act walifika ili asikukatishe tamaa kuwa huwezi Kazi. Alternatively you have a bigger member than she can bear. Jitathmini jibu liko kwako.
 
Aisee tulia upige msosi ndo uandike maana dyuu full mvurugano
 
Hahaha umenena vyema mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…