Tatizo la wanawake kutoshika ujauzito

Mr's goole

Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
17
Reaction score
8

Nipo kwenye ndoa miaka 2 hadi sasa sijawahi kushika ujauzito.

Nimepima vipimo vyote mie na mume wangu hatuna tatizo. Naenda mwezini kama kawaida. Sijawahi kutoa mimba wala kutumia njia yoyote kuzuia mimba. Nimekunywa dawa na kuonana na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake naambiwa sina tatizo. Mume wangu naye hana tatzo.

Huyu ni mwanaume wangu aliyenitoa usichana na amenioa sijawahi kuwa na mwanaume mwingine. Sijawahi kuugua gonjwa lolote la gono. Nipo makini na vyakula ninavyokula.

Nisaidieni mwenzenu kwani nimechanganyikiwa. Sijui inmerogwa? Natamani niende kwa jadi ila naogopa. Tatizo hili ni nini?

WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI


USHAURI/ MAONI YA WADAU

PIA, SOMA:

SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO

Moja ya matatizo yaliyoko katika jamii zetu na yamesababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, ni kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke. Sote tunafahamu kuwa, swala la mwanamke kupata ujauzito linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:

Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko (Menstrual cycle) katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni kuzalishwa katika wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito, pia tatizo la kuwa na uzito wa mwili mdogo sana au mkubwa sana pia huathiri hali nzima ya homoni na kupelekea kushindwa kupata ujauzito.

Umri, kwa wanawake uwezo wa kupata ujauzito unapungua kwa kadri umri unavyoongezeka, hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika wakati umri unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi.

Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), hii husababisha mbegu za kiume (sperms) zishindwe kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utokee. Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, matatizo katika kizazi au upasuaji. Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.

Ute ute katika kizazi (mucus problems), ute unaopatikana katika kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha. Kwa baadhi ya wanawake ute huu unakuwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kuweza kupita, na wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume, haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo ujauzito kutopatikana.

Uvimbe katika kizazi (fibroids), hii huchangia asilimia tatu (3%) katika mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, kwa namna moja au nyingine huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.

Matibabu ya kansa, kwa kutegemeana na aina ya matibabu, aina ya dawa au njia ya mionzi, hizi huweza kumuathiri mwanamke na kumsababishia kushindwa kupata ujauzito.

Ukomavu katika kizazi, kwa baadhi ya wanawake wanayo matatizo ambayo kizazi chao huwa hakijakomaa vizuri au katika kuzaliwa kwao walizaliwa na tatizo hili ambalo, kizazi hakiko sawa (abnormally developed uterus).

Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito yanayo tiba, kama unalo tatizo katika kupata ujauzito usikate tamaa, onana na wataalamu wa afya ili uweze kujua chanzo cha tatizo lako na kupatiwa msaada unaostahili.

Chanzo: tanzlife.co.tz
 
Pole sana mkuu wala usife moyo and keep on trying kuna mtu ninamjua alikuwa na shida kama hiyo ila hakufa moyo na baada ya miaka kumi kazi yake ika-pay off na sasa anae mtoto usife moyo na endelea kuwaona wataalamu tofauti pia angalia hapa chini nime-Google.

 
Pole mdada, najua inatia mawazo sana!nina ushauri mdogo tuu!jamaa huwa hasafiri? Kama akisafiri akae kama mwez hivi, halafu akirud mfanye, tena style ya chuma mboga. Hapo kitanasa tu. Maybe mbegu zinakua hazijakomaa fresh.
 
Duh! Ebana dada pole sana kwa haya majibu unaweza ukajiona upo peke yako au ni jambo la ajabu au ni makosa yako au makosa ya mwenza wako, lakini ukweli ni kwamba haya mambo yapo na fertility za watu zinatofautiana kwahiyo endelea kuwaona wataalamu na endelea kula vyakula bora, supplements na kufanya tendo la ndoa kila ukiwa kwenye ovulation.
 
With Jesus, everything is possible. Believe in Jesus and wait upon HIM. Ni mewaona wengi wenye tatizo kama lako sasa wananyonyesha.As long as dr amethibitisha kuwa hakuna mwenye tatizo kati yenu, basi inahitajika nguvu isiyo onekana! By the way kuna semina ya mtumishi wa Mungu mwl Mwakasege inaanza Jumapili hii pale Kinondoni Biafra kuanzia saa 9 usikose.
 
Pole sana dada, mi naamini siku ikifika mambo yote yatakuwa sawa. Achana na fikra za kwenda kwa waganga, kwani waganga wa jadi wana shida nzito balaa kuanzia shida ya kipesa, stress za kuishi na mashetani/majini, wanafikiria pia nini itakuwa hatma yao pale watakapokufa. yaani kama wataka kuongeza matatizo na msongo wa mawazo jaribu kwenda kwa waganga wa jadi.

Utaishia kutembea na mganga, na hivi umesema uliolewa ukiwa bikra, haha ha ha ha ukienda kwa mganga wa kiume afu aone issue bado inalipa ipo tight, sikufichi utaishia kubeba mimba ya mganga wa jadi.

Tafadhali usinielewe vibaya, The point I am trying to stress here is that don't dare to go to these witch doctors! you will be ripped off then left disappointed!

Chamsingi ni kuendelea na Ibada na ninaamini Mungu atajibu maombi yako siku moja.
 
Mbona miaka 2 michache sana jamani kwa mtu kukata tamaa, utapata tu mpendwa ondoa wasiwasi!
 
Niliwahi kusikia inaweza kutokea ''very rear case' wawili hata wafanyeje(kitaalamu) unless miujiza ya Mungu hawataweza kuzaa lakini kila mmoja aki-divert kwa mtu mwingine atafanikiwa kupata mtoto.

Ni tatizo ambalo kila yai linapokutana na mbegu hufa, hivyo muhimu kumwona specialist aliyebobea.

Nakumbuka kama mwezi na nusu kusoma habari kwenye gazeti la guardian kuhusu wanandoa mtoto wao alishindikana kutibiwa Tanzania ila kuna bingwa india alifatilia historia ya genes za wawili hao hivyo kupata suluhu na kumtibu mtoto.
 

Mpendwa,

Bahati mbaya hujasema uchunguzi uliofanyiwa ni wa aina gani na ulihusisha vipimo gani. tatizo la kutoshika mimba linaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo ya kimaumbile kama hormonal imbalance na hata genetics, ambyayo ukifanya vipimo vya kawaida hakutaonekana tatizo. ni vizuri mkapima pia damu zenu (kama bado hamjafanya hivyo) ili kuainisha vizalia (genes) vyenu, blood proteins na hormonal levels/balance.

Uchunguzi wa mwanzo unaweza kujifanyia mwenyewe kwa kuuchunguza mzunguko wako wa hedhi kama ni regular au irreglar. mara nyingi tatizo la hormonal imbalance huambatana na irregular menstruation circle na timming kati ya peak periods and uterus thickness. kukiwa na mismatch ya hivi vitu, utaweza kushika mimba lakini ikafa baada ya muda mfupi na itakapotoka wewe utadhani ni hedhi kumbe ni miscarriage. kwa kweli naona unahitaji uchunguzi wa kina sana na unaohusisha mambo mengi kwa mapana sana

Kama mchangiaji mmoja (bei mbaya) alivyosema hapo juu, inawezekana kabisa kushindikana mimba kwa baadhi ya couples japo hakuna tatizo lolote bali kwa sababu za viasili vya kimaumbile tu, ila hii ni very rare case! so inahitaji uchunguzi wa kina sana kabla ya kuprove hivvyo.

Hata hivyo, jipe moyo, ondoa wasiwasi na ongeza bidii ya maombi, na Mungu wetu ni mwema na mkarimu sana lazima atajibu maombi yako.

Ubarikiwe sana mpendwa.
 
Hili ni tatizo sugu sasa hivi hapa mjini. Kupata mimba inakuwa ngumu kweli kweli. Ila kule shamba kila mwaka na mtoto wake. Sijui ni ninini hasa tatizo. Hata hivyo, mama usijari inshallah utapata mtoto.
 
Hofu ondoa, mtoto ni majaliwa ya Mungu. Mtangulize Mungu atakusaidia!
 
Let do thz, funga safari uko uliko hadi pale arusha mjn kuna hospital inaitwa St. Thomas muulizie Dr. Msuya, ni specialist wa iyo mambo yakike, shemeji alikaa muda alipofka 2 mambo ikawa poa.
 
Pigeni style ya chuma mboga, hakikisha jamaaa anamwaga mbegu ndaaaniii. Kama vp zifike mpaka mdomoni.
 
Pole sana ndugu yangu sio wewe kilio chako umetuwakilisha wengi kwani hata mi pia swala hilo linanitesa nipo mke wangu bado mambo sio sawa jamani, wenye uelewa na ushauli tunaomba msada hawa wa mawazo.
 
Pole my dear, kama wote wazima labda timing mnakosea. Jitahidi kujua siku zako za ovulation na vile vile labda ute uliokuwa nao ni mkavu hivyo unaweza kuzuia mbegu kufika kwenye mirija.

Unaweza kutafuta Evening primrose oil, hii supplements huwa inasaidia kuweka ute kuwa mlaini ili mbegu zisafiri vizuri kufikia mirija. Vile vile punguza mawazo acha kabisa kuwaza kuhusu mtoto ipo siku utastukia una mimba na jitahidi sana kumuomba Mungu akupe haja ya moyo wako.
 

Miss Jud,

There you are, afanye hivyo.
 
Mwambie mzee ashambulie dakika 90 mfululizo sio anashambulia wiki moja halafu wiki moja analala. ashambulie period mpaka period. Popote akikuona tu akurukie, jikoni, toilet, garden, juu ya magunia ya kolosho, darini, uvunguni, nakazalika. Kama haujapata mimba ndani ya mwezi mmoja basi nachana vyeti vyangu vyote vya mzumbe.

NB: Siku za kupata ujauzito ni chache katika mwezi kama mume ni legelege anashambulia na kupumzika anaweza akawa anazimiss kila mwezi.

Nimemaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…