Tatizo la wasiwasi na njia ya kutibu

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
334
Habari ndugu zangu watanzania.
leo hii nimekuja na makala haya yanayozungumzia wasiwasi na jinsi gani tunaweza kuepukana na tatizo hili.Kwanza kabla ya yote ni kujua ni nini wasiwasi.
Vijana, wasiwasi ni mchakato wa kuchanganyikiwa kwa akili ya mwanadamu unaopelekea vitu vingi kutokea kama vile kutojiamini,kuwa na waoga wa kufanya kitu,kuogopa,kukata tamaa,
kupoteza tumaini,na kushindwa kabisa kujikontrol.

Wasiwasi unasababishwa na mambo mengi sana.Wasiwasi unawezwa sababishwa na msongo mkubwa wa mawazo,pia unaweza sababishwa na viumbe visivyoonekana yaani majini na pia unawezwa sababishwa na kutokana na udhaifu wa afya ya ubongo.

DALILI ZA MTU MWENYE WASI WASI
1.Kujihisi unapenda sana ukimya na kuwa mpweke muda wote.
2.Kujihisi unachanganyikiwa kwa tatizo dogo.
3.Kukata tamaa mapema
4.Kuwa na haraka sana.
5.Kutoweza kunyoosha maneno vyema wakati wa kuongea.
6.Kushindwa kabisa kupata usingizi.
7.Kuogopa mdudu asiyetisha kama vile bui bui au samaki.
8.Kuona kama masikio yameziba na kukuwaka moto.
9.Kulia bila ya sababu ya msingi.
10.Kutoweza kutatua tatizo.
11.Kuanza jambo halafu ukaacha kuendelea nalo.
12.Kujihisi huna umuhimu wa kuishi
13.Kushindwa kujikontroli.

JINSI YA KUONDOA TATIZO
1.Pendelea kunywa maji kwa wingi.
2.Pendelea kunywa maziwa
3.Pendelea kula samaki kwa wingi.
4.Epukana na hali ya upweke tafuta watu wa kukusupport.
5.Pumua kwa nguvu wakati unapohisi wasiwasi
6.Tumia dawa zinazoitwa DIAZEPAM VALIUM
7.Pata muda wa masaa nane ya kulala.
8.Usifanye kazi zinazosababisha kuzidi kwa joto mwilini.
9.Fanya mazoezi kwa mfano kukimbia n.k
 
Hii inanihusu ... Nimechanganyikiwa kwakweli hadi moyo unaenda mbio yaani basi tu .... Yaani nina wasiwasi sio wa nchi hii ... Khaaa ngoja nikanywe maji ya kunywa nikatafute na wa kunipa kampani nishapumua kwa nguvu, samaki wana bei ntakula dagaa, mazoezi kesho...
Asante mkuu
 
thank you too.
Usikate tamaa kila kitu kinawezekana chini ya jua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…