Tatizo langu ni kuwaza kulikopitiliza

danali

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
1,135
Reaction score
1,674
Seriously hili tatizo kubwa linalonisumbua usiku na mchana
Ikufika taim ya kulala kuupata usingizi ni vita kwa kweli na nikishtuka usiku kazi ni ile ile

Sometimes ni tatizo dogo tu ila litakaa kichwani mwangu na kuliwaza sana na hata nikijarubu kupotezea hua nashindwa

Hii inasababisha hata kuniathiri katika shughuli zangu za kawaida

Najaribu kujichanganya na watu ila nikiondoka tu kijiwe hua sina raha tena
Athari ninazohisi zinanisibu
**kupoteza kumbukumbu marakwamara
**kichwa kuuma nafkiri kwa kukosa mda mzuri wa kulala
** mwili wangu unadhoof
** Shughuli zangu haziendi sawa kazini bahati nzuri boss wangu muelewa na anjua nini kinanisibu

Wanajamvi najua wapo watu wamepitia haya au wanajua ni nini Namna ya kufanya ili hali ikae sawa
Naomba ushaur
 
Acha masturbation, ridhika na maisha uliyonayo, kula bamia, asali na toa uchafu masikioni, amka asubuhi na mapema punga upepo, fanya mazoezi, punguza visirani na hasira, mkabidhi Mungu wako maisha yako.
 
Mkuu una tatizo la kisaikolojia linaitwa SONONI, hebu muone pcsycotherapist akusaidie.
 
Acha masturbation, ridhika na maisha uliyonayo, kula bamia, asali na toa uchafu masikioni, amka asubuhi na mapema punga upepo, fanya mazoezi, punguza visirani na hasira, mkabidhi Mungu wako maisha yako.
Suala la masturbation mkuu kwangu limepita kushoto, yaliobaki nitayafanyia kazi
Shukran
 
Depression au hofu inakusumbua, pendelea kucheza Game, km hauna mahusiano ya mapenz fanya hima umpate mwenzio, fanya mazoezi ya viungo kabla ya kulala like Pushup, skwash na mengine ili kuuchosha mwili ulale vzr pia unaweza tafuta movies nzuri uwe unaangalia zinafanya akili iwe busy na kuepuka kuwaza
 
This might be a good solution
 
Kivipi mkuu naomba unieleweshe vizur
Hofu kuto jiamini, kutetemeka na kuumwa kichwa na tumbo kuunguruma chini ya kitovu..

Hofu/msongo wa mawazo unaanzia pale
1. unapowaza hivi nikikamatwa au kuonwa na ndugu, jamaa, au rafiki /mpenzi watanichukuliaje..

2.Pale unapomaliza kitendo na kuanza kujilaumu Kwa nini umefanya hivo wakati uwezo wa kupata mpenzi upo..

3.Mtu huingiwa na Hofu kuu /kutojiamini mbele ya watu wajinsi tofauti na yake Kwa kupatwa na aibu kwasababu tayari ameshakuwa na msongo na tabia ya ubongo hurekodi matukio na hasa yale yanayoonekana/kutendeka mara Kwa mara na yanayosisimua ubongo hasa hivo basi Kwa kuwa kitendo ni cha kuhusu ngono na unapokuwa mbele ya watu mawazo yatakuja ya kingono yakichanganyikana na dhumuni la kuwepo hiyo sehemu, inaweza ikawa dukani, msibani, darasani, kanisani /msikitini hapo ndio hofu huanzia na kupoteza kujiamini kwako.

4.kichwa kuuma hasa maeneo ya nyuma ya kichwa au mbele au pembeni ni kutokana na kulazimisha mzunguko wa damu bila kujiandaa hivo hupelekea sehemu ya ubongo wa mbele na nyuma zinazoratibu hisia kufanya kazi tofauti na Kwa lazima so hiyo hupelekea kuumwa kichwa.
 
Ok asante...vipi kuhusu kutoa uchafu kwenye masikio
 
Ok asante...vipi kuhusu kutoa uchafu kwenye masikio
Unaruhusu masikio kupumua Kwa hewa safi kuingia na kupunguza load ya usikivu na kufika kiurahisi hadi kwenye ubongo, ila sio vizuri kutoa mara Kwa mara ila usiache ujazane kwasababu husaidia kulainisha ngoma ya sikio hivyo kurahisisha kusikia vizuri na ubongo kuweza kupokea na kutranslate Kwa haraka zaidi..
 
Asante maana Mimi ni Muhanga wa hofu kuu mpaka nakua sikai na watu pia situlizani sehemu moja
 
Asante maana Mimi ni Muhanga wa hofu kuu mpaka nakua sikai na watu pia situlizani sehemu moja
Unapiga masturbation,?
Uwe unapiga na zoezi, usisikilize radio au music Kwa earphones kwani ubongo unapata tabu sana..

So mawazo, kuuma kichwa ni tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…