Tatizo ni Umeme? Sukari yaadimika, bei yapaa!

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
530
Wadau, sukari imeanza kuadimika na bei imefika shs 2,000/- per kg. Hali hii inasababishwa na nini? Serikali naona imeamua kuuchuna baada ya awali kuwapiga mkwara wazalishaji na Wafanyabiashara kushusha bei.

Naona hali imerejea kama mwanzo; tatizo nini? Isijekuwa ni sababu ya mgawo wa umeme.
 
Mkuu tangia enzi na enzi yafuatayo huwa ni ya kweli...

Low Supply, causes high demand leading to high prices


Kagera kuna kiwanda cha sukari lakini huko sukari ni kuanzia elfu 3; na sababu kubwa ni kwamba wakipeleka Uganda wanaweza kuuza hata elfu sita..,

Hivyo basi ili kuodokana na hii shida ni kuongeza Supply kwenye viwanda vyetu na kuruhusu watu waingize sukari kwa wingi, kupanga bei kwa serikali kutaongeza tu magendo na serikali kuadimika
 
Mkuu hiyo bei sisi tulishaizoea lakini cha kushangaza jana imepanda mpka 2400 na kuna sehemu mpaka 2600..nilipo ongea na wafanya biashara wakasema, wananunua mfuko wa kg 50 kwa 115,000, hii ina maana wao wana nunua 2300@ 1kg....sijui tunaelekea wapi?.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…