Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Nchi zote duniani kuna masikini (wa kipato) na matajiri wa kipato. Hata siku moja haitatokea kutokuwa na masikini; la sivyo maneno masikini na matajiri halingekuwapo kwenye msamiati (vocabulary) ya mataifa. Na kwa kanuni za kiuchumi masikini wa kipato ndiyo wengi sana wakati matajiri wanapaswa kuwa wachache.
Tatizo linakuja pale tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini inapokuwa kubwa sana, hapo vurugu huweza tokea. Wewe ukute watu kama kumi tu ndiyo wanamiliki karibu pato lote la nchi na mbaya zaidi kama pato hilo wamelipata kwa njia ambazo si halali! Kuna nchi hata hapa Africa watu watatu tu jumla ya fedha wanazomiliki ni sawa na bajeti nzima ya mwaka ya Taifa husika. Tanzania tunaelekea huko. Hii ni hatari sana.
Viongozi wetu wanapaswa kulielewa hili. Wanachotakiwa kukichukia na kukidhibiti si umasikini wa kipato bali ni hii gap kubwa ya kipato kwenye jamii ambayo kwa kweli ni time bomb. Mwalimu Nyerere aliliona hili na kulidhibiti na hii ndiyo iliyochangia kwa kiasi kikubwa amani na utulivu tunaojivunia hadi sasa. Mtu hawezi na wala hatakubali tofauti iliyopo sasa ya kipato: kwa mfano kati ya daktari bingwa na mbunge (hata wa viti maalum) ambaye analipwa mara 40 ya anayopata huyo daktari (ikijumuisha posho na marupurupu, mara 80 ya anacholipwa mwalimu wa sekondari mwenye shahada ya kwanza na kadhalika!!! Kweli hapa tutegemee ni nini? Kusema tu tunauchukia umasikini ndiyo inatosha kweli? Acha hii danganya toto.
Mishahara na marupupu yote ya wanasiasa kuanzia ya raisi inatakiwa kuwa wazi na isipishane na watumishi wengine wa umma kwa mlinganisho wa sifa (qualifications) na madaraka (responsibilities) zao. Ilikuwa hivyo wakati wa Nyerere na ndiyo mabadiliko tunayoyataka.