Tatizo sugu la kutoa usaha kwenye uume

vickboy.com

Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
85
Reaction score
23
Habarini wana JF, mwezenu hivi karibuni nilipatwa na tatizo kiafya, nilikuwa napata maumivu wakati wa kukojoa, usaha ulikuwa unatoka kwenye uume nikaenda zahanati nikawaambia tatizo langu wakanipa doz bila hata kupima nikaanza kutumia.

Baada ya dozi kuisha tatizo likawa palepale japo nilipata ahuen kidogo, wiki iliyopita nikarud tena zahanati na nikaomba kupimwa, kweli nikapimwa mkojo majibu yakaja sina tatizo.

Nikashangaa sana wakati usaha kwenye uume unatoka, basi doctor akanipa dozi tena kwa mara nyingine, nilipewa doxy, cipro na metro hvohvo japo anasema sina tatizo, cha ajabu nimemaliza dozi majuzi lakin still tatizo linaonekana bado lipo maana usaha bado unatoka japo sio kwa mfululizo.

Naombeni ushauri wenu tafadhalini.
 
Pole boss,
Haiwezi kuwa STD kweli?
maana usaha tena hata UTI haipo hivyo.
 
Nenda hospitali, muone Daktari.

Atakushauri ufanye "kalcha & sensitiviti" ya mkojo, pia upime VDRL.

Baada ya ushauri pia pima VVU.

Mche Mola wako, acha uasherati na uzinzi.
 
Ukipewa Dawa, kamilisha dozi.

Ukiandikiwa kununua, hakikisha dawa haijaisha muda wake (expire date),

Pia nunua dawa kwenye duka la kuaminika, kuna maduka mengine huuza dawa feki (bila kujua au kwa makusudi), unaweza kumaliza dozi lakini kumbe ulitumia kitu ambacho si dawa.
 
Nenda hospitali, muone Daktari.

Atakushauri ufanye "kalcha & sensitiviti" ya mkojo, pia upime VDRL.

Baada ya ushauri pia pima VVU.

Mche Mola wako, acha uasherati na uzinzi.

nashukuru kwa ushaur wako!
 

pamoja sana,
 
Mkuu achana na zahanati,nenda hospitali ufanye vipimo,zahanati za sikuhizi ni bure kabisa
 
nenda hospital ya maana achana na hizo zahanati,pia check VVU/HIV.....ol da best
 
pangusa pangusa hyio mkuu,...nenda haraka hosptlal ukapime,usije ukatahamaki pako flat
 
Nenda hospitali tofauti, au labda ni manii na sio usaha. Lini ilikua mara yko ya mwisho kula papuch!!
 

sijambo,shikamoo dokta mkuu
 
Much pole kwako buro!! Ngono zembe ni jatari sana mana mpaka uwe na discharge kwenye sehemu ya siri dat means una STD. La mana nenda kafanyiwe diagnosis ya syphiliss iwe RPR{rapid plasma reagn} au VDRL if nor aggulitination found ndo urudie test ya naisseria gonorroheae,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…