Kwa hali ya kusikitisha maeneo mengi sana ya Tabata yamekumbwa na tatizo la maji, ni zaidi ya mwaka lakini DAWASA imekuwa ikitoa majibu yaleyale kwamba watu wawe wavumilivu huduma itarejea.
Wito waziri afike ajionee msoto wananchi wanaopitia, kuanzia Tabata maeneo ya viwanja vya benki, Segerea kwa mzee Adamu, Segerea Mzimuni, Segerea Migombani, Bonyokwa na maeneo mengine mengi.