Tauhida Gallos Awataka Wanawake Nchini Kujitathimini Ili Kuwa Bora Zaidi Kiutendaji

Tauhida Gallos Awataka Wanawake Nchini Kujitathimini Ili Kuwa Bora Zaidi Kiutendaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

TAUHIDA GALLOS AWATAKA WANAWAKE NCHINI KUJITATHIMINI ILI KUWA BORA ZAIDI KIUTENDAJI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Mhe. Tauhid Gallos Nyimbo amewataka Wanawake nchini kujitathimini kutokana na nafasi walizonazo ili waweze kujua hatua walizofikia kwa lengo la kuwa bora zaidi kiutendaji

Mbunge Tauhida Gallos amewaasa wanawake wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo Mchanga na Mifuko ya Saruji kwa Uongozi wa Skuli ya Kiembesamaki Msingi A iliyopo Wilaya ya Magharibi B tarehe 07 Machi, 2025.

Mbunge Tauhida Gallos Amesema Wanawake Wanafanya kazi nzuri katika nafasi wanazoziongoza ikiwemo ngazi ya familia, Biashara, Ujasiriamali na Uongozi wa Serikali, Taasisi na Vyama vya Siasa.

"Kila mwaka tuna mambo mengi tunayofanya sisi Wanawake lakini baadhi yetu tunashindwa kufanya tathmini, tutumie maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 kujitathimini kwa kujua changamoto na mafanikio ya mwaka uliopita na kupanga kwa mwaka ujao" Mbunge Tauhida Gallos

Aidha, Mbunge Tauhida Gallos amewaomba Wanawake waliobahatika kupata nafasi mbalimbali za Uongozi kuzitumia ipasavyo kwa kuwanyanyua Wanawake wenzao Kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Magharibi kichama, Bi. Fatma Ali Ameir amewataka Wanawake kuzidi kujiamini ili waendelea kushika nafasi mbalimbali za Uongozi.

Bi. Fatma Ali Ameir Amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaamini sana Wanawake kwa kuwapa nafasi za uongozi na hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii, Usawa na Mshikamano ili wazidi kuzidi kuaminika.

Nao, baadhi ya Viongozi wa Skuli ya Kiembesamaki Msingi A wamesema kujengwa kwa sehemu maalum ya kuuzia biashara, kutasaidia katika kudumisha usafi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.10.jpeg
    117.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.11.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.11.jpeg
    113.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12.jpeg
    97.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12 (1).jpeg
    116.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.12 (2).jpeg
    117.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.13.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.13.jpeg
    87.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.13 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.13 (1).jpeg
    104.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14.jpeg
    115.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14 (1).jpeg
    115 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.14 (2).jpeg
    107.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.15.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.15.jpeg
    87.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.15 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-10 at 14.37.15 (1).jpeg
    92 KB · Views: 1
Back
Top Bottom