A
Kama umeshaitwa kazi subiria tu utaitwa kwenda mafunzo ya kijeshi, Anza mazoeziKUBWA KWA WALIOITWA KWENDA KOZI TAWA β TUNAIOMBA SERIKALI ITUSAIDIE!
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona jinsi wenzetu waliopata nafasi kwenye taasisi kama TFS, TANAPA, JWTZ, JKT, POLISI, na Magereza mfano ni taasisi ya TFS wameshaondoka mtaani shida inakuwa nini kwa hawa wa tawa...
Pia wanavyopokelewa kwa heshima, wanapewa taarifa mapema, na kusaidiwa kwa hali na mali katika maandalizi ya kozi zao.
Lakini hali ni tofauti kabisa kwetu tuliopata nafasi kwenye Taasisi ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA). Vijana wetu wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi zikiwemo:
Hii inaleta hisia kwamba TAWA inadharauliwa au haitiliwi maanani kama taasisi nyingine, jambo ambalo linakatisha tamaa vijana walioteuliwa na waliokuwa na ndoto za kulitumikia taifa katika sekta ya uhifadhi wa wanyamapori.
- Kukosa msaada au mwongozo kutoka kwa mamlaka husika.
Tunaiomba TAKUKURU, Tume ya Utumishi wa Umma (PSRS), na vyombo vingine vya serikali:
Kama wazazi wa vijana wa Kitanzania, hatuombi kupendelewa, tunachoomba ni haki, usawa, na mazingira rafiki ya kutimiza wajibu wetu kwa taifa.
- Kufuatilia kwa ukaribu mchakato wa upangaji na maandalizi ya kozi hizi,
- Kuhakikisha kuna usawa na haki kama ilivyo kwa taasisi nyingine za serikali,
- Na kama kuna uzembe, upendeleo au upotoshaji β wachukuliwe hatua stahiki.
Tunaamini serikali yetu kupitia wizara husika italisikia hili na kuchukua hatua haraka.
#TAWA #ChangamotoKozi #TunaombaMsaada #TAKUKURU #Utumishi #HakiKwaWote