JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika kuhakikisha mapato yatokanayo na utalii yanaongezeka, uongozi wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA) umeboresha miundombinu katika maeneo ya utalii.
Kaimu Kamishna wa (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amesema kwa kutumia fedha za bajeti ya maendeleo ya mwaka 2021/22 na fedha za Mradi wa Ustawi wa Taifa na Mapambana dhidi ya UVIKO-19 wametekeleza miradi kadhaa.
Ametaja miradi hiyo kuwa ni; ujenzi na ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 431.4.
Kukamilika kwa ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Lake Natron na katika Pori la Akiba Maswa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Buturi umekamilika kwa asilimia 50.
Ujenzi wa Tourist Bandas saba (7), Campsites sita (6), picnic sites nane (8) na lounge moja (1), ujenzi wa malango na vituo vya kukusanyia mapato saba (7).
Pamoja na ujenzi wa njia ya waenda kwa miguu yenye urefu wa kilometa 1.2.