Tawi La Yanga Lazidi Kupukutika.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
'Tawi la Yanga lazidi kupukutika'.. ndivyo waweza kusema juu ya Singida United ambao ni 'tawi' la Yanga. Hii inakuja baada ya beki wao kisiki, Mganda Shafiq Batambuze kusaini rasmi mkataba wa kuitumikia Gor Mahia hapo jana.

Zoezi hili limekuja baada ya beki huyo kugoma kurejea nchini tangu msimu wa TPL wa 2018/19 ulipoanza kwa kile kinachodaiwa kuwa ni suala la kutolipwa mshahara na kumaliziwa fedha za usajili.

Majanga mengine yanayowakumba Singida United ni;
1. Makocha wake wasaidizi Athuman Mfaume na Jumanne Chale waliachia ngazi kwa sababu ya kutokulipwa mishahara ya miaka kadhaa.
2. Golikipa wao tegemeo, Manyika Peter naye kajiengua katika timu kwa kutolipwa stahiki zake.

Habari bila picha hainogi.. Wale 'matomaso' wenzangu mzigo huo hapo.
 
Wee mwache hajui wachezaji wake wameambiwa mshahara wa mwezi uliopita wautumie vizuri, sijui hill balaa gani linawajia ndugu zetu.
Hahahahahaaaa shabiki wa simba anawayawaya
Wakuu kwani hivyo mlivyoandika, vimeondoa ukweli kua tawi lenu li dhoofu ili hali??
 
Tutaendelea kujuzana yanayojiri katika hili tawi, mpaka pale atakapobaki Mfadhili na Mwenyekiti peke yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…