Tax on Salary goes down from 15% to 14%. Is it Significant enough?

usanii mtupu hakuna lolote kutoka kwenye serikali hii
 
Hawezi kuzikamilisha sasa, labda aseme hata ahidi tena ili azitekeleze awamu ijayo akichaguliwa. Mfano aliahidi umeme wa grid ya Taifa katika maeneo yanayotumia generators mfano Songea. hata kwenye ilani ya CCM utasoma hilo lakini hakuna alichofanya, hata nguzo moja haijachimbiwa wala kuangushwa barabarani toka Makambako kwenda Songea. hata bajeti hii sidhani kama kuna suala la kupeleka umeme huo.

Mkapa aliahidi kuunganisha mikoa ya kusini na kaskazini kwa barabara, alikuwa akikampain Kikwete aliahidi kuendeleza mradi huo mfano barabara ya Mtwara corridor.Toka aingie madarakani mradi huo ndiyo umekufa hata zile file za upembuzi yakinifu uliofanywa kipindi cha Mkapa upo kwenye mafile tu yanapata kutu.

Kikwete aliahidi mambo mengi yanayohitaji gharama kubwa hajatekeleza kabisa, anapiga domo tu.
 
lipi limetekelezwa katika haya? Lipi limewekwa kwenye bajeti hii?
 

Nini kimefanyika katika haya? je bajeti hii itakamilisha haya?
 

Na haya tena!
 
Ahadi kuu kuliko zote na ambayo haijatekelezwa hata kwa 1% ni ya kuleta "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!"
 

Naomba wanaCCM mlete maelezo Serikali ya CCM imefanya nini kutimiza ahadi zake. 2010 ndiyo hii, je? 90%mijini na 65% vijijini wamepata maji safi?
 
Kawakebehi wafanyakazi na kura zao....jana alikuwa anaombaomba kura za wanafunzi Dodoma........kazi kwelikweli
 
Ahadi kuu kuliko zote na ambayo haijatekelezwa hata kwa 1% ni ya kuleta "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!"

ili tuweze kuwapata vizuri tuanze na hizo ndogondogo. Nauliza wamefanya nini? mbona ukisoma ilani sioni walichofanya? kama kipo is not promising at all. Nakumbuka maneno ya Steve Biko (cry freedom) dhidi ya Serikali ya makaburu alipoulizwa 'hakuna kizuri kilicgofanya na Serikali?'
 

Chama kilichojaa porojo, CCM
 
near to zero achievement na bado wanatudanganya. naomba magazeti yaandike hizi ahadi ili kila mtu aone kwa macho yake.
 
Chama kilichojaa porojo, CCM


Teh teh ati kuhamia Dodoma kwanza ni ndoto,

Cha kustahajabisha ni huku wakifikiria kuhamia Dom huku wakati hapo walipo tuuu niwakumbusheni Ule mpango wa kujenga Fly Overz Road zao za Dar kwa taarifa yenu huo mradi upo na umedhaminiwa na serikali ya Japan mkae mjue ivyo sasa niambieni hiyo Dom itakuwepo katika hizo ndoto na porojo zao??

Badala ya kutupa hizo fund kwenda Dom na kuukarabati mji wa Dom na kupunguza purukushani Dar hawataki kabisa hii ni jinsi gani viongozi wetu wa serikali,CCM,manicpl, na wengineo wanao husika na mikakti ya mipango miji walivyo na upeo mchache kabisa kwa Karne hii,

Huyo Kimbisa na kuwa katoke Dom hata kushadadia na kupiga hata porojo za hapa na pale wahamishie hizo Fund Dom walaaa yeye kakaa na kuwazi kupata ubunge Dom Mjini na atangojea sana kama watu wa kondoa hawamtakiiii tuuu sijui, yaaani ni taaaabu kweli kweli.
 
Re: anaepinga apinge tu lkn Ahadi za Jk kutimia: Bajeti 2010/11 mishahara juu

Huyu MS ni wa kusamehewa tu hajui atendalo.
 
Well huu ndio usanii tunaosemaga kila siku walichokifanya ni kutoa na kujumlisha wamepunguza tax kwa minimum wage but wanawaongezea tax kwenye VAT hivyo wanatoa huku wanachukua kule. Mbaya zaidi wameongeza kodi zaidi ya PAYE kuzidi kuwanyonya wafanyakazi. Halafu kuna watu wanadai JK ametimiza ahadi ya kuongeza mshahara mie nawashangaa sana wamesahau ile kodi 15%-14% inawahusu wafanyakazi wenye kima cha chini. Hapo hapo wanasema waziri wa utumishi atatangaza kupandisha mishahara. Tuassume tuna wafanyakazi 20% ni minimum wage wakipandisha mshahara hao wanaoqualify minimum wage ni wangapi? na chukulia mfano mtu alikuwa akipata 150,000 na hakuwa akikatwa kodi, ukimuongezea hadi 350,000 halafu unachukua 30% ya mshahara wake huku kuna makato mengine nayo yanaongezeka je umemuongezea mshahara??.

Kimsingi mie naona hili swala la kodi kwa watumishi liangaliwe upya. Vitafutwe vyanzo vipya vya kodi badala ya kuendelea kumnyonya mtumishi wa serikali kwakuwa ni njia rahisi ya kuongeza mapato. Otherwise, ni kuwaonea watumishi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…