Nilikuwa nawaza kuchukua mkopo ninunue gari niifanye taxi, ila baadhi ya rafiki zangu walishauri bodaboda na kuwa taxi siku hizi hazileti faida kama bodaboda na bajaji. Wadau wenye uzoefu mnanipa ushauri upi?
Mkuu C6 Waliokushauri hivyo walinena vyema kabisa mkuu na ninawaunga mkono kwa sababu kwanza kabisa boda boda ni usafiri wa bei nafuu ambao unaweza kuupata kwa bei nafuu ukilinganisha na gari...huo mkopo wa gari ukiuchukua na ukanunua pikipiki kadhaa na ukapata wafanyakazi waaminifu kwa mwezi unaweza ukajikuta unaingiza zaidi ya milioni moja ukilinganisha na taxi ambapo taxi siku hizi hazina wateja kutokana na gharama ya yake usafiri kuwa juu.
Kama una uwezo wa kuchukua huo mkopo basi wewe chukua na ununue pikipiki kadhaa badala ya gari na ukipata watu waaminifu na ukalenga maeneo yenye watu wengi kama vile chuoni na maeneo ya sokoni utaona faida yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.