Taxify Mtatuua Bodaboda

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Kuna usemi nausikia unasema 'Usipotaka mabadiliko, mabadiliko yatakutaka wewe' kwahiyo maswala ya Uber na Taxify yalipojiri kwa sisi madereva bodaboda sikua na budi kujiunga na mojawapo.

Uber nilishindwa kwakua wana mlolongo mrefu sana.

-Utaambiwa uache nakala ya kadi ya pikipiki.
-Utaambiwa uonyeshe leseni na waihakiki.
-Utaambiwa uache taarifa zako za jinsi unavyopatikana.

Kwanza mimi sina leseni, Hivyo nikaona nikaulize na Taxify.

Wao hawana mambo mengi yaani nilishangaa, hata leseni sikuulizwa. Ni mnakua na mwenyekiti wenu ambaye utakua unaripoti kwake kisha unagewa helmets (ati watu wanatamka element) mbili zenye neno taxify na simu aina ya Nokia One.

Simu inakua na operating system ambayo iko modified na kampuni ili kuendana na jinsi wao wanavyotaka, naamini ni kukutrack zaidi.

Basi bwana.
Siku ya kwanza tangu nianze kua huko Taxify kuna mteja tukawasiliana ikatakiwa nimpeleke Kawe. Hapo tupo Makumbusho, nauli ilisoma shilingi 2500. Baadaye nikapata abiria wa kumpeleka Goba mwisho, tunatokea Makumbusho hapo hapo, nauli ilisoma shilingi 4500.

Nilivyorudi kijiweni nikaingia kwa mama ntilie nikawa na washkaji tukaanza kupiga stori za taxify.
Nikajua kumbe kiukweli ni wenzangu walienda kujisajili taxify kwa ajili ya kupata simu na helmets za bure. Hizo simu walienda kuziflash Kariakoo na kuziuza au kuzitumia wenyewe lakini hakuna aliyejisajili akiwa amedhamiria kuifanya kazi.
Hiyo ni kutokana na sifa mbaya za Taxify zilizoenea.

Nikazima data siku nzima.

Jana jioni nikawasha data. Kuna binti akarequest nikiwa Oysterbay ili twende Ubungo nikarespond nauli ikakadiriwa kua ni 3500, akiwa hajapanda akaanza kuongea na mimi, mimi nikabonyeza kuonyesha tumeshaanza safari. Akaongea na mimi zaidi ya dakika tano kisha akapanda lakini akawa hajui njia, tukazunguka eneo moja kama mara mbili.

Kutoka hapo nikawa kila eneo lenye zebra nasimama na kwenye traffic lights nasimama (Sijawahi kutii sheria kama jana) mpaka tunafika Ubungo nauli inasoma 7500.
Dada alilalamika nusura anibonde, ananiuliza mbona ilimkadiria kua nauli ni 3500 imefikaje huko? Mimi nikajibu kupungua au kuongezeka kwa nauli kunategemea foleni na muda nitakaotumia barabarani.

Tatizo ninaloona ni chombo kutembea umbali mkubwa na kukongoroka wakati hela haiji nyingi ya kutosha kuhudumia chombo na maisha yangu

Lakini pia wateja nao wamejanjaruka, wameshajua taxify na uber ni sadala, yaani taka usitake kwa boda boda kujiunga na taxify au uber kuna kipindi itafika itakua ni lazima siyo ombi.
Mpaka huo muda ukifika ngoja nifanye mpango wa kuwarudishia vitu vyao, sijajisikia vyema kuipata hiyo hela kwa njia ya wizi kiasi hicho.
 
Last week nilikuwa namsindikiza mtu kituo cha mawasiano nkakuta jamaa wa taxify bodaboda kapasua helmet kapata abiria kutoka gongo la mboto mpk mawasiliano kalipwa buku 3
 
Last week nilikuwa namsindikiza mtu kituo cha mawasiano nkakuta jamaa wa taxify bodaboda kapasua helmet kapata abiria kutoka gongo la mboto mpk mawasiliano kalipwa buku 3
Taxify ni tatizo, mi simlaumu. Siku hizi mafuta ya 2000 hawauzi wanaanzia 3000 kwahiyo huyo jamaa kapata hela ya mafuta safari ndefu kama hiyo.
 
sasa si muachane nao
Kwa kipindi hiki hiyo ni option. Abiria nao wameichangamkia Taxify kwakua imeleta bei ambazo ziko favourable mno kwa upande wao.
Kwahiyo 80% wakiijua na kujiunga taxify kinachobaki inakua ni lazima dereva ujiunge Taxify pia.
 
Nawapenda taxfy sana
Kuna siku nilirequest wanifate kwangu wanipeleke banana ukonga wakaniambia elf 14 kabla niliwaita uber wakaniambia elf 30 ilibidi nicancell uber

Nilichokuja kugundua baadae kumbe uber walinicharge mara mbili kuna siku niliwaita hawajaja kwahiyo wakataka kufidia safari ambayo sijaenda sababu hawakuja
 
Hata mimi ningekua abiria Taxify ingekua ndiyo suluhisho langu la usafiri na ningeipenda kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…