Taxify, Kampuni inayokuwa kwa kasi Ulaya na Afrika katika huduma ya usafirishaji imetambulisha huduma mpya ya ‘TaxifyBomba’ maalum kwa magari madogo, Dar es Salaam, Tanzania.
Kampuni hiyo inajaribu kupanua chaguzi za wasafiri na kuruhusu madereva wa magari madogo ambayo yanatumia mafuta kwa matumizi madogo kujipatia fursa ya kipato.
Taxify Bomba ni daraja rafiki kwa jamii kutokana na nauli ndogo na faida kubwa kwa madereva. Daraja hili linahusisha magari madogo yenye viti vinne ya kuanzia 1300cc kushuka chini.
Haya ni magari yenye injini ndogo ambazo hutumia mafuta kidogo, na kusababisha gharama za uendeshaji kuwa chini kwa madereva na hivyo kuwezesha utoaji wa huduma kwa bei nafuu kwa wasafiri.
Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji nchini Tanzania alieleza kuwa, “Tumebaini kuwa, soko la wateja wetu linapanuka. Kwa sasa watu wamefikia mahala ambapo wanataka chaguzi nyingi zaidi za usafiri na jinsi wanavyoweza kufanya safari zao ndani ya jiji. Pia kuna ongezeko kubwa la madereva ambao wanataka kutumia magari yenye injini ndogo. Huduma hii inakidhi mahitaji ya madereva na watumiaji.
Katika kutambulisha huduma hii ya Taxify Bomba, Taxify imetoa punguzo la asilimia 30 ya fedha ambapo nauli itaanzia sh. 800, sh. 210 kwa kilomita moja, sh. 50 kwa dakika na usafiri wa chini sh.2,000.
“Bei za daraja hili zimeundwa kwa uangalifu wa hali ya juu ili kuwapa nafasi wasafiri kwenda popote ikiwa ni fursa moja wapo pia ya kuwawezesha madereva kupata zaidi. Madereva watakuwa na nafasi ya kufanya safari nyingi kupitia daraja hili jipya,” alielezea Remmy.
Taxify imeongeza uvumbuzi zaidi na kuelewa mahitaji ya madereva na wasafiri wanaotumia huduma hiyo.
Taxify Bomba inatambulishwa ikiwa ni miezi michache tu baada ya uzinduzi wa TaxifyBajaji (chaguo la usafiri wa Bajaji) na Taxify XL (magari yenye viti sita).
----/----
Kuhusu Taxify
Taxify inaongoza Ulaya kwa kutoa huduma ya usafiri kupitia mtandao, imekuwa ikiwaunganisha mamilioni ya wasafiri na madereva Duniani katika kurahisisha huduma ya usafiri, kwa haraka na ufanisi zaidi.
Ufanisi wa Taxify na teknolojia yake umesaidia uendeshaji wa biashara ya kisasa na kuwanufaisha madereva ambao ulipa kamisheni kidogo pamoja abiria kulipa nauli ndogo.
Ilihasisiwa na Markus Villig, Taxify ilizinduliwa mwaka 2013. Hii ni miongoni mwa kampuni za utoaji huduma za usafiri mtandaoni ambayo inakuwa kwa kasi Ulaya na Afrika. Hapa Tanzania, Taxify inatoa huduma Dar es Salaam na Mwanza.
Taxify ina watumiaji zaidi ya milioni 10 katika nchi zaidi ya 25 ulimwenguni. Zaidi tembelea;
www.taxify.eu
MWISHO