Warrior Codes Brand
New Member
- Apr 27, 2024
- 2
- 0
Taxpayers Shop ni nini?
Huu ni mfumo wa mtandaoni nilioubuni kwajili ya kuhamasisha na kushawishi watu wote wa ngazi zote na biashara zote kuweza kulipa Kodi muda wote wanaponunua au kuuza bidhaa au huduma ya aina yoyote
Mfumo huu una lengo la kutengeneza msingi na kupanua wigo wa ulipaji Kodi ili kuongeza mapato katika Taifa letu.Ni mfumo unaofaa kutumika popote pale Duniani na katika kila Taifa lenye uchumi wa ngazi tofauti kuanzia zilizoendea,zinazoendelea na hata maskini.
Nimeubuni Mfumo huu ili kila mwananchi afurahie kulipa Kodi kwa hiari na kupunguza mianya ya ukwepaji Kodi ambalo ni janga la Ulimwengu.
Mfumo huu unafanya kazi Kwa mtu yoyote ambaye ana risiti halali ya manunuzi aliyoyafanya awali,ambapo atatakiwa kutuma namba za hiyo risiti ili aweze kupata nafasi ya kujiunga kununua bidhaa yoyote inayopatikana katika Duka mtandao letu la Taxpayers Shop kwa punguzo la kuanzia asilimia 10 na kuendelea.
Duka letu hili la mtandaoni litakuwa na bidhaa zote zinazotumiwa na binadamu na litakaribisha muuzaji wa bidhaa yoyote halali kuweka bidhaa yake humo kwajili ya mauzo, na Bei ya bidhaa yake lazima iwe na punguzo la kuanzia asilimia 10 au kuzidi.
Kila risiti moja itatumika kununua bidhaa mara moja na haitatumika Kwa mara nyingine
Bidhaa zote zinazopatikana zitaonyeshwa katika Duka mtandao letu pamoja na Bei zake zikiwa tayari na punguzo la asilimia 10 au zaidi
Baada ya kununua bidhaa yoyote katika Duka mtandao letu mnunuzi atapatiwa namba ya utambulisho(code)ambayo ataitumia kupata bidhaa yake aliyoinunua
JINSI MFUMO HUU UNAVYOFANYA KAZI
Mfumo huu ni mkusanyiko wa maduka mengi na maelfu ya bidhaa na huduma zinazopatikana Kwa mteja kwajili ya mahitaji yake ya Kila siku
Mteja atakuwa na uwanda mkubwa wa uchaguzi wa bidhaa na huduma,anachotakiwa kufanya ni kujisajili kwa kutuma namba za risiti aliyofanya malipo na kuweza kuingia katika mfumo wa manunuzi ndani ya Duka mtandao ambapo atapata punguzo hilo kwa bidhaa yoyote atakayohitaji
NANI ANAFANYA MFUMO HUU UWE HAI NA KUFANYA KAZI VYEMA
Ili mfumo huu uweze kufanikiwa na kuwa imara anatakiwa awepo muuzaji wa bidhaa na mnunuzi wa bidhaa hizo. Mnunuzi atavutiwa kutumia Duka mtandao hili(Taxpayers Shop)kwa sababu ya punguzo kubwa la Bei za bidhaa zinazopatikana humo
KWANINI TUNAANZISHA MFUMO HUU WA TAXPAYERS SHOP
Ili Serikali yoyote iweze kuendelea lazima kuwe na idadi kubwa ya wananchi wanaolipa Kodi ambapo watachangia mapato na hivyo kukuza uchumi wa Taifa.
Ili kufanikisha hilo Kuna haja ya kubuniwa mbinu mbalimbali za kuwahamasisha wananchi katika kishiriki kulipa Kodi na hii ni njia mojawapo ya muhimu.
Mfumo huu utawafanya wananchi wafurahie kushiriki kulipa Kodi kwa hiari yao kwa sababu kwa kulipa Kodi huko watapata faida ya ya kupata mapunguzo ya bidhaa na huduma zozote katika matumizi yao ya Kila siku kutoka katika Duka mtandao.
Malipo ya bidhaa na huduma kutoka katika Duka mtandao hili yatafanyika mtandaoni kwa njia mbalimbali kama Tigo pesa,M pesa,Halopesa, Airtel money,PayPal, Credit cards,Bank transfer na nyinginezo zitakazofaa
MUDA GANI DUKA MTANDAO LINAKUWA WAZI
Mfumo huu upo hewani muda wote,bidhaa na huduma zinapatikana bila kikomo Cha muda wala msimu
NI WAPI LINAPOPATIKANA DUKA MTANDAO
Mfumo huu unapatikana mahali popote ni baada tu ya mtumiaji kujisajili kwa upande wa muuza bidhaa au huduma na pia Kwa upande wa mnunuzi wa bidhaa au huduma
HUDUMA ZA KUONGEZA THAMANI (VALUE ADDED SERVICES) ZA TAXPAYERS SHOP
Katika kuboresha mfumo na kuongeza kuvutia ushiriki wa watu wengi,Mfumo utakuwa unafanya na kuendesha huduma zifuatazo:-
I)BAHATI NASIBU YA TAXPAYERS SHOP
Kila mwisho wa wiki washiriki 20 wenye bahati wataweza kujinyakulia zawadi na pesa taslim 100,000 Kila mmoja
Jinsi ya kushiriki ni kwa anayependelea ni kutuma namba ya risiti (ambayo alitumia kujisajili)katika sehemu maalum ya bahati nasibu iliyopo ndani ya mfumo wetu ambapo washiriki watashuhudia moja kwa moja mtandaoni namba zao za risiti zikichaguliwa kwa zilizopata bahati ya kushinda
Mshiriki ataruhusiwa kutuma idadi yoyote ya risiti ili kujiongezea nafasi za ushindi
II) MASSE(MAKE SCIENCE SUBJECT EASY)
Hii ni kampeni maalum ndani ya mfumo wetu yenye lengo maalum la kuimarisha na kuinua masomo ya Sayansi kuanzia Shule ya msingi hadi sekondari kuhakikisha unazalisha wanaSayansi Bora Duniani
Kutakuwa na vipindi vya masomo ya Sayansi ufundishaji Bora kutoka kwa wafundishaji mahiri na wabobezi (kinadharia na kimatendo) na bunifu mbalimbali Bora za kisayansi kutoka kwa wabunifu wetu wazawa ili kuwaunga mkono kwa bunifu zao na kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi
Mafundisho yote hayo yatapatikana kwa Bei ya punguzo la asilimia kumi na yatakuwepo muda wote kwa mwanafunzi kuyafuatilia,Mtandao una mfumo ambao hautaruhusu kurushiana kimtandao masomo hayo,kila mhitaji atapakuwa ya kwake
III) TAXPAYERS SHOP ART GALLORE (T PASSAGE)
Hili ni Dirisha linalopatikana ndani ya mfumo wetu linalomwezesha kila msanii/mbunifu kuweka kazi yake na kuuza kwa faida kubwa kuliko mtandao wowote Duniani. Mfumo umetengeneza utaratibu ambapo msanii ataweka bidhaa yake ili wateja wake waweze kuipata kwa urahisi sana kwa kuinunua kwa kiasi kidogo tu Cha sh 500/-,Ambapo baada ya kufanya malipo mteja ataipata kazi hiyo lakini hataweza kuwatumia watu wengine ili Kila mmoja aweze kununua ya kwake.kazi inaweza kuwa katika mfumo wa picha,maandishi au video
Dhumuni kuu la kuweka dirisha hili la (T PASSAGE) ni kuwapa nguvu,thamani na malipo Bora wasanii ili kufidia jasho lao katika kufanya ubunifu wa kazi mbalimbali
FAIDA ZA TAXPAYERS SHOP
Upande wa mnunuzi:Atapata uwanda mkubwa sana wa machaguzi wa bidhaa na huduma za kununua bila kupata usumbufu wa utafutaji
Usalama: Bidhaa zinazopatikana humu ni halali zenye ubora na usalama kwani zitadhibitiwa na mamlaka husika za serikali
Punguzo: Mnunuzi atafaidika na ununuzi wa bidhaa yoyote kuanzia asilimia 10 na kuendelea
Upatikanaji: Ni njia rahisi ya kupata bidhaa na huduma zinazohitajika
Bahati Nasibu na Zawadi: Mnunuzi atakuwa na nafasi za kushinda pesa taslim kila wiki kwa ushiriki wake kwenye dirisha la bahati nasibu
Upande wa Muuzaji: Ni sehemu Bora ya uuzaji wa bidhaa na huduma na yenye mzunguko wa biashara kwani ni sehemu inayotembelewa na idadi kubwa ya wanunuzi. Ni sehemu ya kutangaza,kufanya masoko na kuuza bidhaa na huduma zote wakati mmoja kwa ufanisi mkubwa
Mauzo kwa haraka: Mlipa Kodi (mnunuzi)atafika haraka hapa kwajili ya Bei ya kuvutia ya punguzo la asilimia 10 au zaidi. Ni Duka lisilofungwa na lisilo na mhudumu bali lina huduma muda wote: Bidhaa ikishawekwa hapa tayari ipo sokoni kununuliwa na mteja.
Upande wa Serikali:
Wazo kuu la mradi huu ni kuongeza idadi kubwa ya walipa Kodi,itavuta walipaji wa chini kabisa ambao ni wengi kwani itawezeaha hata wenye biashara ndogo kutamani kushiriki katika mfumo huu kwani una faida nyingi kwao.
Kupunguza ukwepaji Kodi: Watu wataongezeka kuwa walipa Kodi wazuri kwani mfumo ni rafiki na wenye faida
Kuimarika kwa miundo mbinu: Mfumo utaongeza mapato kwa serikali hivyo itaweza kuboresha miundo mbinu nchini
Kudhibiti Uhalifu wa Kodi: kwa sababu mfumo unapokea risiti halali za malipo itapunguza wafanyabiashara wanaotoa risiti zisizo halali na hivyo kuikosesha mapato serikali. Kodi kwa maendeleo ya Taifa: Nchi yenye walipa Kodi wengi ina maendeleo makubwa
Andiko hili limelenga kuingia kwenye kinyang'anyiro ili lipate nafasi ya kuweza kutumika na kufanikisha kusudio la kuleta maendeleo ya muda mrefu ndani ya Taifa letu na hii ndio Tanzania tuitakayo ndani kipindi Cha miaka 5-25 na hapo mbeleni

Upvote
2