Bado sana jengo la kuonesha ukuu wa serikali linatakiwa kuwa na aina fulani ya kukabiliana na mafuriko, vurugu na muonekano.
Msingi wa jengo ulitakiwa unyanyuliwe juu zaidi ili hata kukitokea mafuriko madogo jengo la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Polisi , Jengo la Mahakama, Jengo la Hospitali , kituo cha reli na shule za serikali yawe majengo ya mwisho kabisa kukabiliwa na mafuriko ktk eneo lote la kata au wilaya.
Turudi katika jengo hili la Mkuu wa Wilaya tunaona mapungufu ikiwemo msingi wa jengo hauja nyanyuliwa kuwa juu kupita majengo yatakayoizunguka ofisi hii hapo siku za usoni na si ajabu likizungukwa na majengo au ukuta tu tayari litakaribiwa na adha ya mafuriko ya maji madogo.
Ukiangalia wasanifu wa majengo muhimu niliyoyataja tukiangalia majengo ya mjerumani, mwingereza, mchina TARAZA utaona majengo yote yana msingi mrefu sababu kubwa ni kuondokana na adha ya mafuriko madogo, kuleta taswira ya nguvu / mamlaka ya taasisi , nafasi ya kutolea habari/ taarifa kwa umma ktk ngazi ndevu mbele ya jengo au kujikinga uvamizi wa watu wenye hasira n.k