Elections 2010 Tazama picha hizi, kisha jipange kupiga kura 2010, Au Wasemaje?

Elections 2010 Tazama picha hizi, kisha jipange kupiga kura 2010, Au Wasemaje?

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Ebu tazama picha hizi kwenye blog moja na jiulize utampigia mgombea yupi kati ya hawa tunaowana kwenye maeneo yetu

gonga hapa
 
Hahahaaa, nimeipenda zaidi hii. Kasi mpya nguvu mpya ari mpya. Najiuliza hivi ile kasi ilikuwa ni ya kwenda wapi vile? Sasa hivi wamekuja na kasi zaidi ari zaidi nguvu zaidi! Hapa najiuliza ya kufanya nini? Nawashangaa wanaoipapatikia CCM.

kasi+mpya+1.bmp
 
Ebu tazama picha hizi kwenye blog moja na jiulize utampigia mgombea yupi kati ya hawa tunaowana kwenye maeneo yetu

gonga hapa

Mkuu yapo mazito na ya huzuni zaidi ya hayo. Ila kwa sababu ya vitisho, umaskini, njaa, kutoifahamu haki ya kidemokrasia basi wananchi vijijini wanajua kuwa ukihongwa ni lazima umpigie kura aliyekuhonga maana atajua kuwa hukumpigia. Inatakiwa tuwaeleweshe wananchi kuwa pokea hongo, kula kwa mrija wakati wa kupiga kura hakuna anayejua kuwa hukumchangua fulani maana hatuandiki majina.

Hahahaaa, nimeipenda zaidi hii. Kasi mpya nguvu mpya ari mpya. Najiuliza hivi ile kasi ilikuwa ni ya kwenda wapi vile? Sasa hivi wamekuja na kasi zaidi ari zaidi nguvu zaidi! Hapa najiuliza ya kufanya nini? Nawashangaa wanaoipapatikia CCM.

kasi+mpya+1.bmp
...Jana :confused2:JK ameahidi kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa misenyi kule bukoba kama akichaguliwa tena kuongoza nchi...:confused2::confused2::confused2:
 
Kama wewe ni mzazi au mzalendo halisi, basi itakubidi ukapimwe akili kama utairudisha madarakani kwa kura serikali inayondesha mambo yake kama hivi katika karne ya 21 kwenye nchi isiyo na vita na iliyosheheni rasilimali za kutosha
 
Attachments

  • kasi mpya 4.jpg
    kasi mpya 4.jpg
    12.3 KB · Views: 42
kuna watu wanasamba uongo huko vijijini kuwa ukiwapigia kura wapinzani utajulikana na utachukuliwa hatua, sasa watu wanaolishwa uongo huo kwa vile hawana hata elimu wanaogopa kupiga kura kwa wapinzani eti watafahamika na kuchukuliwa hatua kali na viongozi wao mi vijiji .
 
Hao wananchi hawahitaji Shule nzuri wala madawati ya kukalia,wao wanahitaji fulana,kofia na kanga doti moja, na ahadi nzurinzuri zinazovutia wasikilizaji. Nadhani serikali yao iwe ya kijiji, kata au ile kuu,inavutiwa na hali hii kwa vile inawasaidia kuvuna wapiga kura wengi,wanapowamaskinisha watu, wanawafanya kuwa waoga zaidi na kuwa royal kwao, fikiria hao watoto kama hawatakwenda sekondari,watabaki kijijini kusubiri siku mbunge wao anapokuja na kuwanunulia debe la pombe ya kienyeji,watamnadi kuwa anawajali kweli.
 
Nawashauri CHADEMA wachukue hizi picha watengeneze mabango, wayaweke sambamba na yale ya JK! Uchaguzi huu si kwa ajili ya JK na tabasamu lake bali ni juu ya watanzania na mustakabali wa maendeleo yao. Huu ndio ujumbe wa picha hizi kufunika ule wa mashindano ya ulimbwende unaonyeshwa na mabango ya CCM!
 
kuna watu wanasamba uongo huko vijijini kuwa ukiwapigia kura wapinzani utajulikana na utachukuliwa hatua, sasa watu wanaolishwa uongo huo kwa vile hawana hata elimu wanaogopa kupiga kura kwa wapinzani eti watafahamika na kuchukuliwa hatua kali na viongozi wao mi vijiji .

ukusanywe ushahidi juu ya hilo, halafu CCM wakishinda matokeo yapingwe kwa madai kwamba CCM walitumia mbinu chafu ya kupiga kura. Nilishangaa kwamba kule Kiteto CCM walikuwa wanaonyesha picha za mauaji ya Kenya na kudai eti wakichagua upinzania yatawakuta yale, lakini upinzani hata hawakuipeleka CCM mahakamani. Kuanzia sasa itabidi haki hii itafutwe kwa nguvu. Tukishindwa mahakamani tutatumia upinde na mishale.
 
...Jana :confused2:JK ameahidi kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa misenyi kule bukoba kama akichaguliwa tena kuongoza nchi...:confused2::confused2::confused2:

yaani alikuwa hana hata touch na wananchi wa huko wanataka nini, kwani wao shida yao kubwa ni Maji... sasa hicho kiwanja kitarusha ndege za kuleta maji au?! kwanza hata walikuwa hawaielewi hiyo hoja ya uwanja wa kimataifa kwani haiwahusu...
 
Back
Top Bottom