SoC03 Tazama ramani utaona nchi nzuri

SoC03 Tazama ramani utaona nchi nzuri

Stories of Change - 2023 Competition

2Laws

Member
Joined
Sep 4, 2022
Posts
37
Reaction score
38
"Tazama ramani utaona nchi nzuri

Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka

Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,

Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania..."

Ningetamani kuimba hata mwisho lakini wengi tunaufahamu na tumewahi imba. Ila nilikisudia tuvute taswira na kuyatafakari maneno ya wimbo huu ili ninaposema Tanzania ni kisima cha utajiri tuelewane kwa urahisi.

Kwanini nafikiri Tanzania ni kisima cha utajiri? kama ni tajiri mbona haitajwi pamoja na nchi kama Uswizi, Norway, Uchina, Marekani n.k. miongoni mwa nchi zilizoendelea? Yanaweza kuwa sehemu maswali Unayotafutia majibu. Fuatana nami unaweza pata jibu lako.
Nikitaja utajiri kuna vitu muhimu vitatu ambavyo hutambulisha utajiri na nina uhakikaTanzania tunavyo;

Amani. Utajiri namba moja ambao Tanzania tunajivunia ni amani. Haihitaji kutumia nguvu sana kueleza hali ya maisha katika nchi kama Libya, Sudani na Afrika kutokana na migogoro ya kisiasa na ugaidi. Unajua kwamba tunaweza kulala, tunaamka na kwenda kufanya shughuli zetu kwasababu kuna amani. Tunawapokea wawekezaji kutoka nje kwa sababu hatuna vita. Amani inatuwezesha kufanya shughuli zetu za kila siku.

Ardhi. Nikitaja ardhi nasemea kuanzia vyanzo vya maji na hifadhi yake yote mpaka mlima Kilimanjaro. Tanzania ina jumla ya eneo la Mha 94.5 za ardhi, ambapo Mha 44 zimeainishwa kuwa zinafaa kwa kilimo. Kati ya ardhi inayolimwa inayopatikana ni Mha 10.1 tu au asilimia 23 ya ardhi inayolimwa kwa sasa, bado 77% zipo tuu. Karibu 6.5% ya Tanzania ni maji, maziwa makubwa Afrika, mito na mabwawa kwa uvuvi, usafirishaji, uzalishaji wa umeme na kilimo cha umwagiliaji. Mlima mrefu zaidi Afrika, Serengeti na hifadhi kubwa zenye vivutio vya utalii, n. K. Sijasemea machimbo ya vito vya thamani ambavyo vyote vipo katika ardhi ya Tanzania weka na Tanzanite ipatikanayo Tanzania pekee japo hifadhi kubwa na soko kubwa linaongozwa na India.

Watu/nguvu kazi. Tuna zaidi ya watu milion 65 huku kama 61% yake ni vijana. Maana yake nguvu kazi yakutosha kabisa kama tukiamua kupiga jembe.

Sasa waweza shangaa mbona kama tuna kila kitu tunachohitaji kuwa nchi yenye maendeleo zaidi hapa Afrika na duniani!? Nini kimepunguka? Majibu yanaweza kuwa mengi. Wanasema kisicho mkononi mwako si chako mimi nimetaja vile ambavyo bado tunamiliki, baada ya kupata uhuru wetu vilikuwa vyetu na wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza ni wetu.

Sisemi ukabila, Mwalimu alikataa, ila Wachaga mnisaidie; una ng'ombe wako na kaja mgeni ananjaa, utampa ng'ombe umwambie bwana, mpe chakula, mpe dawa na mtunze akizaa; nigawie mazaiwa kidogo? Najaribu kusema kwamba watanzania tumekuwa watu wakukaa pembeni tukisubiri waje wawekezaji walime, waweke mbolea kwenye shamba letu, watie maji; wakivuna ndipo watukatie sehemu ya mavuno kama shukrani.

Hayati Mwalimu Jk Nyerere alisema "madini yetu hayaozi, tuyaache huko huko, mpaka watanzania watakapokuwa na ujuzi wa kuyachimba ili tunufaike wenyewe na vizazi vyetu",

Najifunza vitu viwili hapa; kwanza Aliamini ili tunufaike na rasilimali zetu lazima tuwe wawekezaji wa ndani, na pili alitazamia elimu tutakayoipata isiwe kujua kusoma ma kuangika tuu, bali namna tutakavyoweza jinufaisha na rasilimali zetu, yaani elimu na vitendo.

Labda tutazeme kwa picha nyingine, tafakari juu ya maana ya "uzalendo" kama maana yako inasehemu inayotaka uwajibikaji basi tuko pamoja, si uwajibikaji kwa tumbo tuu, bali kwa familia, jamii na hata taifa. Ninajaribu kusema kila mtanzania ananafasi ya kuijenga Tanzaniaa iliyoendekea bila kujali umri, jinsi ama nafasi yake.

Ni habari ya kusikitisha unapoona kijana mtanzania hata tu kupiga kura ya kuchagua kiongozi anapuuzia tuu; kwanza hafuatilii sera gani atatumikia miaka mitano ijayo, pili hapigi kura mpaka kuwepo na hongo na ahadi za upendeleo na tatu hajui msimamo wa siasa katika nchi yake ukoje. Nukuu "Siasa ni jambo zito sana kuwaachia wanasiasa, na Charles de Gaulle" sina hakika kama tunaifahamu.

Sasa twende kwenye shughuli za kijamii na maendeleo, kama mwenyekiti si mjanja kuliko, vijana hata waona.
Kitu kimoja nilijifunza katika awamu ya tano, Kama kila mtanzania atawajibika kufanya kazi, iwe kwa hiari ama kulazimishwa maendeleo yataonekana tena kwa kasi. China wanajituma kutengeneza treni za kasi ili watu wa wahi katika kazi maana wao waliota ndoto kama ya Mhe Hayati John Pombe Magufuli; Aliamini katika kazi na nadhani aliondoka mapema akidhani watanzania tulimuelewa. Ni kweli tulimuelewa? Vijana hatujarudi tena vijiweni asubuhi? hatujaanza kulewa tena asubuhi?

Changamoto nyingine bado siasa yetu ni hafifu, kuna vitu kama tungelitilia mkazo basi kungekuwa na mabadiliko makubwa. Mfano Kilimo kwanza/ kilimo ni uti wa mgongo tungekuwa moja ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mazao zaidi ya matano duniani.

Naweza ipongeza awamu ya tano Tanzania imetajwa namba mbili katika nchi zinazofanya vizuri zaidi katika utalii Afrika.

Nihitimishe kwa tafakari, Je kuna tofauti kati ya;
"Hapa kazi tuu" na "na kazi iendelee"?

Marejeleo: Maphill, volza. Com, yieldgap. org, Google search

1690664773096.png
 
Upvote 1
"Tazama ramani utaona nchi nzuri

Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka

Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,

Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania..."

Ningetamani kuimba hata mwisho lakini wengi tunaufahamu na tumewahi imba. Ila nilikisudia tuvute taswira na kuyatafakari maneno ya wimbo huu ili ninaposema Tanzania ni kisima cha utajiri tuelewane kwa urahisi.

Kwanini nafikiri Tanzania ni kisima cha utajiri? kama ni tajiri mbona haitajwi pamoja na nchi kama Uswizi, Norway, Uchina, Marekani n.k. miongoni mwa nchi zilizoendelea? Yanaweza kuwa sehemu maswali Unayotafutia majibu. Fuatana nami unaweza pata jibu lako.
Nikitaja utajiri kuna vitu muhimu vitatu ambavyo hutambulisha utajiri na nina uhakikaTanzania tunavyo;

Amani. Utajiri namba moja ambao Tanzania tunajivunia ni amani. Haihitaji kutumia nguvu sana kueleza hali ya maisha katika nchi kama Libya, Sudani na Afrika kutokana na migogoro ya kisiasa na ugaidi. Unajua kwamba tunaweza kulala, tunaamka na kwenda kufanya shughuli zetu kwasababu kuna amani. Tunawapokea wawekezaji kutoka nje kwa sababu hatuna vita. Amani inatuwezesha kufanya shughuli zetu za kila siku.

Ardhi. Nikitaja ardhi nasemea kuanzia vyanzo vya maji na hifadhi yake yote mpaka mlima Kilimanjaro. Tanzania ina jumla ya eneo la Mha 94.5 za ardhi, ambapo Mha 44 zimeainishwa kuwa zinafaa kwa kilimo. Kati ya ardhi inayolimwa inayopatikana ni Mha 10.1 tu au asilimia 23 ya ardhi inayolimwa kwa sasa, bado 77% zipo tuu. Karibu 6.5% ya Tanzania ni maji, maziwa makubwa Afrika, mito na mabwawa kwa uvuvi, usafirishaji, uzalishaji wa umeme na kilimo cha umwagiliaji. Mlima mrefu zaidi Afrika, Serengeti na hifadhi kubwa zenye vivutio vya utalii, n. K. Sijasemea machimbo ya vito vya thamani ambavyo vyote vipo katika ardhi ya Tanzania weka na Tanzanite ipatikanayo Tanzania pekee japo hifadhi kubwa na soko kubwa linaongozwa na India.

Watu/nguvu kazi. Tuna zaidi ya watu milion 65 huku kama 61% yake ni vijana. Maana yake nguvu kazi yakutosha kabisa kama tukiamua kupiga jembe.
Sasa waweza shangaa mbona kama tuna kila kitu tunachohitaji kuwa nchi yenye maendeleo zaidi hapa Afrika na duniani!? Nini kimepunguka? Majibu yanaweza kuwa mengi.
Wanasema kisicho mkononi mwako si chako mimi nimetaja vile ambavyo bado tunamiliki, baada ya kupata uhuru wetu vilikuwa vyetu na wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza ni wetu.

Sisemi ukabila, Mwalimu alikataa, ila Wachaga mnisaidie; una ng'ombe wako na kaja mgeni ananjaa, utampa ng'ombe umwambie bwana, mpe chakula, mpe dawa na mtunze akizaa; nigawie mazaiwa kidogo? Najaribu kusema kwamba watanzania tumekuwa watu wakukaa pembeni tukisubiri waje wawekezaji walime, waweke mbolea kwenye shamba letu, watie maji; wakivuna ndipo watukatie sehemu ya mavuno kama shukrani.

Hayati Mwalimu Jk Nyerere alisema " madini yetu hayaozi, tuyaache huko huko, mpaka watanzania watakapokuwa na ujuzi wa kuyachimba ili tunufaike wenyewe na vizazi vyetu",

Najifunza vitu viwili hapa; kwanza Aliamini ili tunufaike na rasilimali zetu lazima tuwe wawekezaji wa ndani, na pili alitazamia elimu tutakayoipata isiwe kujua kusoma ma kuangika tuu, bali namna tutakavyoweza jinufaisha na rasilimali zetu, yaani elimu na vitendo.

Labda tutazeme kwa picha nyingine, tafakari juu ya maana ya "uzakendo" kama maana yako inasehemu inayotaka uwajibikaji basi tuko pamoja, si uwajibikaji kwa tumbo tuu, bali kwa familia, jamii na hata taifa. Ninajaribu kusema kila mtanzania ananafasi ya kuijenga Tanzaniaa iliyoendekea bila kujali umri, jinsi ama nafasi yake.

Ni habari ya kusikitisha unapoona Kijana mtanzania hata tu kupiga kura ya kuchagua kiongozi anapuuzia tuu; kwanza hafuatilii sera gani atatumikia miaka mitano ijayo, pili hapigi kura mpaka kuwepo na hongo na ahadi za upendeleo na tatu hajui msimamo wa siasa katika nchi yake ukoje. Nukuu "Siasa ni jambo zito sana kuwaachia wanasiasa, na Charles de Gaulle" sina hakika kama tunaifahamu.

Sasa twende kwenye shughuli za kijamii na maendeleo, kama mwenyekiti si mjanja kuliko, vijana hata waona.
Kitu kimoja nilijifunza katika awamu ya tano, Kama kila mtanzania atawajibika kufanya kazi, iwe kwa hiari ama kulazimishwa maendeleo yataonekana tena kwa kasi. China wanajituma kutengeneza treni za kasi ili watu wa wahi katika kazi maana wao waliota ndoto kama ya Mhe Hayati John Pombe Magufuli; Aliamini katika kazi na nadhani aliondoka mapema akidhani watanzania tulimuelewa. Ni kweli tulimuelewa? Vijana hatujarudi tena vijiweni asubuhi? hatujaanza kulewa tena asubuhi?

Changamoto nyingine bado siasa yetu ni hafifu, kuna vitu kama tungelitilia mkazo basi kungekuwa na mabadiliko makubwa. Mfano Kilimo kwanza/ kilimo ni uti wa mgongo tungekuwa moja ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mazao zaidi ya matano duniani.

Naweza ipongeza awamu ya tano Tanzania imetajwa namba mbili katika nchi zinazofanya vizuri zaidi katika utalii Afrika.

Nihitimishe kwa tafakari, Je kuna tofauti kati ya;
"Hapa kazi tuu" na "na kazi iendelee"?

Marejeleo: Maphill, volza. Com, yieldgap. org, Google search

View attachment 2702522
Maendeleo hayaji yenyewe, yanatafutwa, na hayakawii pale palipo na bidii na ufahamu. Nitafurahi kama utakubaliana nami
 
Back
Top Bottom