Unaona sasa... kumbe kweli ulini-miss halafu husemi kwamba ulini-miss! Mwenzako ilikuwa nikiku-miss nakuja nakuchungulia, kisha huyoooo... kimya kimya, sikusemeshi wala sikuulizi ingawaje kuna siku ilibaki kidogo tu... nikaona wale waliokuwa wanashuhudia picha la Kihindi wanaweza kushitukia, kwamba eh, kumbe Amitabh Bachchan!!Hahahahaaaa uwiiiiiiii!Ujue nimecheka sana!Nilikua najiuliza huyu mtu kaenda wapi?
Mbona huyu chige anafanana kimtazamo naye?
Nikagundua ndio wewe,wewe!
Unaona sasa... kumbe kweli ulini-miss halafu husemi kwamba ulini-miss! Mwenzako ilikuwa nikiku-miss nakuja nakuchungulia, kisha huyoooo... kimya kimya, sikusemeshi wala sikuulizi ingawaje kuna siku ilibaki kidogo tu... nikaona wale waliokuwa wanashuhudia picha la Kihindi wanaweza kushitukia, kwamba eh, kumbe Amitabh Bachchan!!
Hamna cha life ban wala nini... hilo la kunijua, ni kwavile tu nimeamua nisibadilishe sauti; vinginevyo; achana na mimi bhana! Nikiamua nile chimbo; unaweza kunitafuta karne mzima na usinione... kijana wa kiume usishangae kukuta naongea sauti ya bibi kizee; nachanganya miherufi mikubwa na midogo humo humo, na penye kuandika neno ustaarabu wala sioni taabu kuandika ustalabu ili mradi tu usinijue!Hahahaaaa poleeee,hata hapa wenye akili watakua wameshakujua.
Vipi naona umepigwa life ban?...lol
Kulikoni???
Hamna cha life ban wala nini... hilo la kunijua, ni kwavile tu nimeamua nisibadilishe sauti; vinginevyo; achana na mimi bhana! Nikiamua nile chimbo; unaweza kunitafuta karne mzima na usinione... kijana wa kiume usishangae kukuta naongea sauti ya bibi kizee; nachanganya miherufi mikubwa na midogo humo humo, na penye kuandika neno ustaarabu wala sioni taabu kuandika ustalabu ili mradi tu usinijue!
Fella mchizi wangu... tena sana tu... long time kitambo hata Bongo Flavor haijaanza!! Lakini kibongo bongo, uki-mess na Fella; umeumia... bora u-mess na Ruge! Nakumbuka enzi za Wanaume Family, maskani madogo walikuwa wanamuogopa kama ukoma... wakianza kumng'ong'a basi ni lazima wafanye hivyo kimachale machale kwa imani kwamba Fella alikuwa anawaandea kwa bibi! Siku nimemuona Fella nyoko ni pale alipozinguana na mmoja wa washikaji wa Wanaume Family... kwa ku-show love, watu tukam-support yule mchizi akaenda studio, akagonga kopi kibao... nakumbuka tulihangaika sana kusambaza ile album radio stations...hata hivyo, haikupata airtime kabisa! Wambeya wakatupenyezea habari kwamba Fella kapita kufukia nyayo kila tulipopita... mchizi ambae tulimpa support ni very talented lakini amebaki historia!!
Hata hivyo, Fella sio mshamba kihivyo, sema inawezekana akinyuka pamba hazimtoi! Long time alikuwa na tabia ya kuvaa vijinzi vya kubana... ingekuwa siku hizi tungeita model... pata picha na ule mwili wake ingawaje enzi hizo hakuwa vile!!!
Thubutu... hebu anza na hint nikusikie!!!duuuuuuuuuhuuu!!!!!!
wewe sijui km sikujui!
Tena kwa mimi mtu ninayemjua Fella enzi tunamuita Saidi, wala siwezi kumuelewa mtu akisema Fella ni mshamba! Fella long time dah, sina hata cha kusema... alipoona Bongo haisomeki, akazama kwa Madiba... kule nako hakutaka kujisahau na kuona amefika mwisho wa reli, akaamua kurudi tena Bongo na tangu arudi, amekuwa aki-mprove kimichongo mwaka hadi mwaka!!kiukweli fella kwa muonekano ni mshamba sana ila jamaa ni bonge la mjanja la kupanga mawazo kuwa pesa....siyo leo jamaa janja wayback kabla halijatoka dizonga na kuja bongo na kuanza kupiga mpunga kwenye music kwa kuanzia na juma nature!
washaanza wivu hao... hapo tu, sijanyuka suti zangu... nikishazinyuka watu si watasimama mapigo ya moyo; kuona eh, hili jamaa lisharudi lianze tena kumsarandia Ifa!Kuna tatizo kwani?
huyo ndo aliyeandika "happy birthday my son shamira" kwenye page yake ya insta.... Jamaa wakampa makavu sema daughter huyo ni mtoto wa kike akafuta fasta!!
Huyo ndo aliyeandika "happy birthday my son shamira" kwenye page yake ya insta.... Jamaa wakampa makavu sema daughter huyo ni mtoto wa kike akafuta fasta!!
Nimekuwa nikitizama shughuli za mziki tanzania nkagundua kuna miungu watatu, Ruge, Said fella na babu tale. Hawa jamaa wana ka cartel kao, ukigombana na mmoja unapotea kabisa. Ila wana sifa zinazofanana nitawaletea mfululizo wa makala ila nianze na Fella Saidi.
Hajui kabisa kuvaa ni mshamba aliwahi kwenda Ikulu pale na jeans na tshirt juzi nimemuona kumbe alirudia zilezile kwenye tuzo za Diamond Channel O.
In short the guy ni mshamba anavaa mapete makubwa yana rangi rangi km mganga wa jadi nmeona video akiwa na diamond wanachukua tuzo alikera.