Makampuni ya simu huwa na kawaida ya kukodi ardhi kujenga minara kutokana na survey zao. Upangaji huu ungekuwa fursa nzuri kuongeza kipato kwa baadhi ya wazee maskini ambao ardhi yao imeonekana inafaa kuweka mnara wa simu. Mara anatokea mtu ooh natafuta eneo hili niweke mashine, hivyo niuzie eneo hili. bila kujua kitu gani nkiko nyuma wazee hawa huuza kipande cha ardhi kwa wajanjanja hawa. wiki mbili tatu unaona mnara huo unajengwa. wazee hawa maskini wamedanganywa.
Hawa watu ambao hununua ardhi muda mfupi kabla ya mnara kujengwa hupewa taarifa hizi na nani?
Je, inawezekana ni makampuni yenyewe huwa yanapanga hii hujuma
Jamani huu si wizi ambao unapaswa kupingwa.
Mfano mzuri ni mnara uliojengwa Mwandama, Kata ya Sapiwi Bariadi. huyo mzee anamaisha magumu mno, nilipomuuliza alimuuzia nani, hata hajui anasema walikuja kutoka mjini wakanunua , wiki moja baadae mnara ukaanza kujengwa.
KWA MTAZAMO WANGU HUU NI WIZI WA KUPINGWA KKWA NGUVU ZOTE.