TAZARA - Rais Magufuli tunakuomba utupie jicho uongozi hili shirika

TAZARA - Rais Magufuli tunakuomba utupie jicho uongozi hili shirika

Ladydii

Member
Joined
Dec 17, 2019
Posts
83
Reaction score
159
Mheshimiwa rais na serikali yako tunaomba uitupie macho TAZARA.

Kumekua na utendaji mmbovu mnoo na kwa muda mrefu kwenye hii taasisi.

Watendaji wakuu wamekua chanzo cha migogoro na mazingira magumu kwa wafanyakazi na wateja.

Shirika limejaa urasimu unaoharibu utendaji bora wa watendaji wa chini na wateja, hii inasababisha kuwa na huduma mbovu sana na kupoteza mapato mengi sana kama nchi.

Tazara wanafanya kazi kwa mazoea bila kufuata taratibu.

Wafanyakazi hawana vitendea kazi muhimu kadri ya mahitaji ya kazi zao, kitu kinachofanya utendaji kuwa mbovu na kazi kutofanyika kwa wakati.

Watumishi wanafukuzwa kazi bila kufuata taratibu kitu kinachoishia kuja kuligharimu shirika na kuzitesa familia zao.

Watumishi wanabambikiwa madeni kwa visingizio vya shirika kutopata taarifa zao muhimu kama imprest retirements za miaka mingi bila kusikilizwa.

Management mbovu kwenye safari za safari zimekua mbovu siku baada ya siku, wateja wanaingia gharama kulala vituoni kwa gharama kubwa sababu ya uzembe.

Niseme kwamba kanaweza kuwa na mawili; kwanza inawezekana uongozi wa tazara hauna nia dhati ya kuboresha shirika zaidi ya wakubwa kujinufaisha wenyewe kitu ambacho ni hujuma au, mbili uongozi wa tazara ni mbovu na umeshindwa kafanya ulichotakiwa kufanya na unahitaji kuondolewa na kuweka uongozi mpya.
 
Kwa kweli kama zile SDD 20 yani niliingia workshop mbeya kiukweli zimeanza kuisha kabisa. Zina failure vibaya sana. Na spare hawanunui.

Ila mkuu ishu ya management ni tatizo linalosumbua hata upande wa pili huku. Sasa huwa najiuliza hizi taarifa huwa hazifiki kweli kwa wahusika wakuu wa nchi kujua mienendo ya haya mashirika?
 
Tazara ni Kati ya Yale mashirika yanayohujumu juhudi za serikali ya awamu ya tano.

Tazara wamejisahau mno wenyewe wanajionaga kwamba wako nje ya serikali, wanajifanyia kazi holela tuu, hawana mipango yoyote ya kuboresha huduma zao, hawaboreshi office, hawajali maslahi ya watumishi, hawajali wateja halafu wanaona hakuna hatua wanayoweza kuchukuliwa.

Ni kama vile shirika ni mali ya mkurugenzi na watu wake wachache, au ni kama vile mkurugenzi ameshindwa kazi na amebaki kuendeshwa na watu wachache huku watumishi waliowengi wakipambana na hali zao wenyewe na wateja wakiteseka.

Wakati rais anapambana kuboresha miundombinu wenyewe wanapambana kuua miundombinu iliyotayari.

Wizara husika washughulike na hawa watu kabla hawajaliua shirika
 
Back
Top Bottom