TB Joshua hakupendwa na wahubiri wenzake

TB Joshua hakupendwa na wahubiri wenzake

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Baada ya kuwazidi nguvu na kanisa lake kufurika watu, wahubiri wenzake wa Nigeria walimchukia TB Joshua bila sababu ya msingi.

Licha ya kutompenda lakini alizidi kuwa moto wa kuotea mbali duniani kote, kama ilivyokuwa kwa Magufuli hapa Tanzania baada ya wanafiki Chadema kujitokeza kutompenda hata kama wanapita kwenye flyover na ndege alizonunua yeye.

Pia soma > Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia

-----
Imeelezwa kuwa TB Joshua aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57 alikuwa miongoni mwa wahubiri wakubwa nchini Nigeria ambaye hakukubaliwa na wenzake licha ya kuwa na wafuasi wengi barani Afrika.

Alitengwa na Chama cha Wakristo wa Nigeria (CAN) na Wapentekoste wa Nigeria (PFN) huku sababu mbalimbali zikitajwa licha ya kuwa hakuwa tofauti na wahubiri wengine waliokuwa wakihubiri katika televisheni na kuwateka raia wa Nigeria tangu mwanzoni mwa miaka ya 90.

“Joshua ambaye alikuwa kiongozi wa kanisa la Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) hakuwa mmoja wao. Alikuwa mkali. Hakuogopa lolote. Njia zake hazikuwa za kawaida," amesema Abimbola Adelakun, profesa msaidizi katika idara ya mafunzo katika Chuo Kikuu chaTexas.

Joshua alianza mahubiri kwenye televisheni miaka ya 90 na wafuasi wake walimuona kama mtu wa kuaminiwa na mnyenyekevu na ujumbe wake ulienea duniani kote.

"Hawaamini kwamba unaweza kujisimamia mwenyewe bila kuwa na mtu wa kumtegemea," amesema Gbenga Osinaike, mchapishaji wa taasisi kuu ya uchapishaji wa vitabu ya Kanisa la Kipentekoste nchini Nigeria.

TB Joshua aliyezaliwa Juni 12, 1963 anatajwa kama mhubiri ambaye hakutumia nguvu katika shughuli zake za kiroho lakini maombi yake yalionekana kuwa na nguvu.

"Watu walikuwa na fikra akilini ya jinsi ambavyo Mungu angefanya kazi na walipoona kitu tofauti kutoka kwake wakaamini zilikuwa ni nguvu hizo.”

“Walitumia 'muujiza' sawa wa leso, waliuza mafuta sawa ya 'upako' na maji matakatifu ambayo waliamini kuwa yaliponya magonjwa yote na picha zao zilichorwa kwenye fulana na vijikaratasi vilivyotumiwa na wafuasi wao. Lakini kwa sababu hakuwa katika kundi au katika tafsiri yao ya vile wanavyomuona Mungu, alitengwa na kusemwa vibaya ," amesema Osinaike.

Amesema TB Joshua alishutumiwa na wachungaji wenzake kwa kubuni miujiza bandia, na kudai kuwa mchungaji huyo aliwajibu kuwa miujiza hiyo ilikuwa ya kweli akisisitiza kuwa alichokuwa akifanya TB Joshua pia kilikuwa kinafanywa na wachungaji wengine ambao hawakupingwa na watu waliowaamini.

Mwaka 2004, mamlaka ya usimamizi wa matangazo nchini Nigeria ilipiga marufuku vituo vya televisheni kupeperusha matangazo ya miujiza ya wachungaji moja kwa moja kwenye televisheni.

Iliaminiwa kuwa Joshua ndiye anayelengwa, kwamba wachungaji hasimu walikula njama ili Serikali iweke marufuku hiyo kwa sababu alikuwa ametawala vyombo vya habari.

"Huenda alikuwa ndiye mchungaji wa kwanza kutumia matangazo kupitia intaneti kunadi mahubiri yake kwa watazamaji kimataifa ," amesema Adelakun.

Amesema kuwa tofauti na wachungaji wengine, TB Joshua

hakuanzisha matawi ya kanisa lake katika kila kona ya mtaa na mara nyingi familia yake haikuhusishwa na kazi yake, mke wake alionekana mara chache karibu naye na hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefahamika kuongoza kanisa lake.

Kwa sasa kanisa lake limefungwa huku wanajeshi wakiimarisha ulinzi kutokana na mamia ya waumini kujaa wakilia na kuomboleza.

"Ilikuwa ni kazi na maisha ya mtu mmoja, ingawa alikuwa na mitume wake. Ni vigumu kuona kanisa likiendelea bila yeye," amesema Osinaike.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwamba?

"kama ilivyokuwa kwa Magufuli hapa Tanzania baada ya wanafiki Chadema kujitokeza kutompenda hata kama wanapita kwenye flyover na ndege alizonunua yeye."

😂😂😂😂😂😂😂!

Haya waambieni wasiokuwa na macho wala masikio.
 
Hivi unajua kwa nini Taifa la Israel linachukiwa sana na watu waovu?
Ni kwa sababu ya AGANO lake na Mungu.
Nimejaribu kukupa picha tu kidogo
Ila elewa ukiona mti unapigwa mawe ni kwa vile umebeba Matunda
Ukiwa Mtumishi wa Mungu alafu ukajikuta shetani anakupenda jua wewe ni Mtumishi Agent wa Shetani na ndio wengi sasa
Wanadamu wanakuona Mtumishi lakini katika ulimwengu wa Roho unamtumikia shetani kwa siri
Joshua hakujichanganya ndio maana wengi walimchukia
 
Akifufuka mnaweza bisha mpaka kiama kwamba ilikuwa movie.Nilimkunali Sana TB Joshua natamani Mungu afanye muujiza amrejeshee pumzi.
 
Baada ya kuwazidi nguvu na kanisa lake kufurika watu, wahubiri wenzake wa Nigeria walimchukia TB Joshua bila sababu ya msingi.......

Licha ya kutompenda lakini alizidi kuwa moto wa kuotea mbali duniani kote, kama ilivyokuwa kwa Magufuli hapa Tanzania baada ya wanafiki Chadema kujitokeza kutompenda hata kama wanapita kwenye flyover na ndege alizonunua yeye...
Ulianza vizuri habari yako ,ili kuna jina umelitaja hapankwenye paragraph za kwanza kwanza ,nikaishia hapo hapo kusoma,nikajua habari yako siyo credible
 
Chadema muda huu wanatafuta nitoke vipi kwa nguvu zote
Majuzi nilimsikiliza mbowe bada ya hiki kifo anatia huruma siutani yani Ni fedheha

Chadema Ni wakupambana na diamond na kupachika kiki bada ya kifo cha TB
 
Wakati naanza kusoma uzi wako nikataka kushangaa yaani uanzishe uzi bila kuwataja Chadema?

Ila hata hivyo umejitahidi sana hadi mwisho wa uzi wako hujamtaja Mbowe leo! Umeanza kukua Elitwege
Yaani huyu mtu, alijiunga hapa JF kwa ajili ya kumsifia na kumtukuza Mwendazake, na kuinanga CDM na Mbowe wake tu! Yaani hana jipya!
 
Hivi unajua kwa nini Taifa la Israel linachukiwa sana na watu waovu?
Ni kwa sababu ya AGANO lake na Mungu.
Nimejaribu kukupa picha tu kidogo
Ila elewa ukiona mti unapigwa mawe ni kwa vile umebeba Matunda
Ukiwa Mtumishi wa Mungu alafu ukajikuta shetani anakupenda jua wewe ni Mtumishi Agent wa Shetani na ndio wengi sasa
Wanadamu wanakuona Mtumishi lakini katika ulimwengu wa Roho unamtumikia shetani kwa siri
Joshua hakujichanganya ndio maana wengi walimchukia
Huwa naogopa sana kumtetea mwanadamu yeyote kwani uhalisia huwa anaujua mwenyewe
 
Back
Top Bottom