ALIYEKUWA mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Twiga Cement, Leon Hooper amedai kuwa bei ya mfuko wa saruji haiwezi kushuka na kuwa Sh5,000. Hooper, ambaye amekuwa kwenye biashara ya saruji kwa zaidi ya miaka 25 maeneo mbalimbali duniani, ameeleza kuwa anakubaliana na wazo kuwa sementi ishuke bei hapa nchini, lakini akasema ahadi hizo hazitakiwi kuwa za haraka na ambazo hazina mchanganuo akisema kuwa zinaweza kuuchanganya umma kuhusu bei halisi ya bidhaa hiyo. Hooper ameeleza kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji ambazo ni kati ya dola 50 hadi 80 za Kimarekani kwa tani moja ikitegemea na sehemu ambayo simenti hiyo inapelekwa, zinafanya suala hilo kuwa gumu.
"Nimesikia kuwa kuna vyama vinatoa ahadi kuwa vitashusha bei na kuwa 5,000 katika maeneo kama Mara, Songea na Mwanza, kitu ambacho hakiwezekani kutokana na utaalam wangu," alieleza Hooper. Katika mikutano yake mbalimbali, mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa amekuwa akiwaambioa wananchi kuwa serikali yake itahakikisha bei ya saruji itashuka hadi kufikia Sh5,000 kwa mfuko na pia kushusha bei ya vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi waishi kwenye nyumba bora badala ya zile za nyasi na udongo.
Dk Slaa alisema bei hizo zinawezekana kushuka kwa kuwa serikali yake itaondoa kodi zote za bidhaa hizo. Hadi sasa bei ya simenti ni kati ya Sh1,2500 hadi Sh1,300 jijini Dar es salaam wakati mikoani bei inafikia hadi Sh1,700 kwa mfuko. Lakini simenti inayotoka nchi kama Pakistan ambayo iko maelfu ya kilomita kutoka Tanzania, inauzwa kwa bei hiyo ya Sh1,250 sawa na simenti inayozalishwa nchini. Mmoja wa wauzaji hao ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa bei ya jumla ya saruji ya hapa nchini kwa Twiga ni Sh 11,900 na ya Pakistani ni Sh 11,800 lakini ikiingia mtaani huuzwa kwa bei moja ya Sh 12,500. Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Viwanda, Biashara na Kilimo(TCCIA), Mhandisi Aloyce Mwamanga alisema upangaji wa bei za vitu huendana na gharama za uzalishaji wa bidhaa hiyo.
Akizungumza na Mwananchi juzi, Mwamanga alisema kuwa lengo la mfanyabiashara na mzalishaji yeyote ni kupata faida hivyo ni vigumu kuuza bidhaa kwa bei ya hasara iliyo chini ya mstari wa uzalishaji. "Unataka niuze viazi kwa Sh200 wakati gharama za uzalishaji ni Sh300?, Hilo haliwezekani.
Unajua 'price'(bei) ya 'commodity' (bidhaa), lazima iendane na gharama ya uzalishaji," alisema. Alifafanua kuwa: Lazima uweke gharama zako za uzalishaji, baada ya kuweka gharama hizo za uzalishaji, ndipo utaje bei itakayokupa faida ili kesho uzalishe tena. "Mimi sijiingizi katika siasa, lakini, kama utauza saruji kwa Sh5,000 na gharama za uzalishaji zipo chini ya hapo, Ok," alisema Mwamanga.
Suala la saruji kuwa bei juu nchini lilizengumziwa mwaka jana na katibu mkuu wa Umoja wa Wazalishaji wa Saruji Afrika Mashariki (EACPA), Harpreet Duggal aliyeeleza kuwa kodi zinazotozwa na serikali kwa makampuni ya sementi Afrika Mashariki ziliwekwa ili kulinda viwanda vya bidhaa hiyo dhidi ya ile ya nje ambayo huzalishwa kwa gharama za chinikutokana na makampuni kupewa ruzuku na serikali zao. Akizungumza na gazeti la The East African ambalo ni gazeti dada la Mwananchi, Duggal alisema Tanzania imeathirika kwa kiasi kikubwa na saruji kutoka Pakistan ambayo imetawala soko kwa asilimia 15.
"EACPA inafikiria sana maendeleo haya na tuna wasiwasi kuhusu maendeleo ya viwanda vya saruji Afrika Mashariki kama jumuiya haitachukua hatua zinazofaa," alisema. Mtendaji mkuu wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Charles Mbogori alisema akiwa Arusha kuwa kuingia kwa wingi kwa saruji ya bei rahisi kutoka nchi zinazozalisha kwa gharama ndogo, kutaleta matokeo mabaya kwa viwanda vya ndani baada ya muda.
Mbogori alisema kuwa viwanda vya ndani vinakabiliwa na gharama kubwa za uzalishaji zinazotokana na gharama kubwa za umeme, wafanyakazi na mtandao mbovu wa usambazaji haswa usafirishaji wa reli Alisema kuwa miundombinu mibovu na umbali kati ya viwanda vya saruji na wateja pia ni chanzo cha gharama kubwa za uzalishaji. "Serikali za EAC zinatakiwa kuangalia njia nyingine ya kupata umeme wa bei rahisi ili kufanya biashara ya saruji kuwa ya ushindani," alisema.
Saruji ni moja ya bidhaa ambazo ni nyeti hivyo katika suala la kodi imewekewa asilimia 55 mwaka 2005 ambayo ilikuwa kupunguza kiwango cha asilimia 5 kwa mwaka na kuifanya ifikie asilimia 35 kwa mwaka 2009. Hata hivyo, Juni 2008 unyeti katika sekta ya saruji liliondolewa na uingizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ulipunguzwa kutoka asilimia 40 hadi asilimia 25.
"Kitu hiki kilifanywa bila mawasiliano na wadau katika biashara ya saruji," alisema Mbogori.
CHANZO>>
MY TAKE:
CCM
😛uke: