TBC imekosa usawa hadi kwa yanayoonekana dhahiri

TBC imekosa usawa hadi kwa yanayoonekana dhahiri

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
TBC wanayo matangazo kipindi hiki ambayo yanahamasisha watu kwenda kupiga kura. Matangazo haya yanakuwa na kipande cha mtu anaongea kuhamasiha wengine kwenda kupiga kura na ni matangazo yasiyofungamana na chama chochote.

Sasa limekuja la 'Mhogo Mchungu' maarufu kwa uigizaji wa filamu. Tangazo la Mhogo Mchungu lina 'Background sound' ya wimbo wa Zuchu unaitwa Tanzania ya Sasa ambao ni wimbo maarufu wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi, nyuma yake kuna jengo lenye rangi ya njano na kijani aidha ni ofisi ya CCM au Yanga na mwisho Mhogo mchungu anamalizia kwa misamiati yake na kuuliza kwanini uende kuchuma mboga ambako hukujui? amewataka watu wakachume ambako wanakufahamu na japo hamfundishi mtu wa kupigia kura lakini akili kumkichwa.

Wanachofanya wanaweza kuwa wanakiumiza chama tawala kuliko kukisaidia, kuna watu wanapiga kura ya unyonge kwa kumsaidia anaeonewa, kuna watu hawapendi makelele ya kitu kimoja, kuna watu wanaopenda haki na usawa nk.
 
TBC wanayo matangazo kipindi hiki ambayo yanahamasisha watu kwenda kupiga kura. Matangazo haya yanakuwa na kipande cha mtu anaongea kuhamasiha wengine kwenda kupiga kura na ni matangazo yasiyofungamana na chama chochote......
TBC ya Ryoba ni taasisi ya hovyo zaidi nchi hii, Lissu akiingia madarakani siku 100 za kwanza timua viongozi wote na watangazaji ukianza na yule anaejiita Elizabeth mramba
 
Back
Top Bottom