Wanabodi,
Wale wenye access, naombeni muangalie TBC, kuna kipindi live cha majadiliano kikiendeshwa live kutoka Dodoma kikiongozwa Mtangazaji wa TBC Dodoma, Victoria Patrick akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali, ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Mwananchi, huku mjadala ukichangiwa na watangazaji wa TBC Dar es Salaam.
Mjadala huu ni very healthy kipindi hiki cha janga la Corona,
Habel Chidawali ametoa changamoto ya msingi sana inayavikabili vyombo vya habari katika kipindi hiki cha janga la Corona, amesema kuwa ingawa vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa mstari wa mbele kuripoti updates za ugonjwa wa Corona zinazotolewa na serikali, kitu kinachotakiwa zaidi na jamii ya Watanzania sio updates tuu ya wagonjwa wangapi, bali utoaji wa elimu ya kinga dhidi ya maambukizi, kwenye hili la elimu, vyombo vya habari, bado havijatimiza jukumu hili kikamilifu, hivyo there is still so much to be done.
Pia Habel Chidawali amezungumzia changamoto ya maambukizi inayowakabili waandishi wa habari katika kipindi hiki cha janga la Corona. Amesema waandishi wa habari ni kama wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Corona, wenzetu wahudumu wanapewa kinga, kwenye media bado hakuna media inayowapa waandishi wake vifaa vya kujikinga, hivyo waandishi kujikuta wako kwenye hatari ya kuambukizwa, na kueleza hata hiyo ya social distancing ya kukaa umbali wa mita moja, kwa waandishi imeshindikana, ukifika tuu mahali ukijulikana ni mwandishi, watu wanakuzonga kwa karibu.
Chidawali amevisisitiza vyombo vyote vya utangazaji kutumia mic za boom stick kwa waandishi wake, na waandishi wote wanapaswa kuvaa face mask wakati wote wawapo kazini.
My Take.
Kwa vile na mimi ni mwandishi, naomba nichangie kidogo.
- Kwanza niipongeze Mkurugenzi wa TBC Dr. Ayiub Rioba kwa mabadiliko chanya ya Aridhio na kuipongeza TBC kwa mjadala huu, pili nimpongeze mtangazaji Victoria Patrick kwa kuongoza vizuri mjadala na kumpongeza Habel Chidawali kwa mchango mzuri.
- Pili nivipongeze vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya uhabarishaji umma, na utoaji wa elimu ya jinsi ya kujikinga na Corona, na hapa naomba kutoa pongezi za ziada kwa jf, kama chombo cha pekee cha habari kinachoongoza kwa uhabarishaji umma.
- Niipongeze serikali kwanza kwa ku limit watoa habari za update ya Corona, ni watu 5 tuu, Rais, VC, PM, Waziri wa Afya na Msemaji Mkuu wa Serikali, hapa naomba kutoa shukrani za pekee kwa Afisa Habari wa Serikali, Zamaradi Kawawa ndie husambaza zile updates za serikali, sijui kwa kipindi hiki huwa unalala saa ngapi, anaamka saa ngapi na anachoka vipi maana updates ni kila dakika!.
- Naomba kumpongeza kwa dhati kabisa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas kwa kuwa reachable nakushiriki katika vipindi mbalimbali vya uelimishaji umma, pia kwa kunipatia access ya reaching out viongozi wowote wa serikali kutoa elimu kwa umma na alianzia kwa Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile.
- Naomba kumpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa daily update, hadi Corona ikimalizika, huyo Ummy atunukiwe tuu shahada ya udakitari maana atakuwa tayari amehitimu udakitari kamili balo tuu kuingia internship.
- Pamoja na pongezi hizo zote, kwenye reaching out strategies, Tanzania as a nation bado, hakuna muongozo wowote wa kitini chochote cha elimu ya kinga ya Corona kwa umma. Kwenye main stream media bado kuna kazi kubwa ya kufanywa katika utoaji elimu, media zinazotoa elimu ya kinga ni kwa media hizo kujitolea na sio obligation. Kwenye janga kama hili, jukumu la utoaji wa elimu ya kinga lisiachiwe kwa media pekee as option kwa kujitolea, bali jambo hili liwe ni obligation kwa Wizara ya Afya, kutengeneza vipindi vya elimu kwa umma kwa kuwatumia wataalamu wake, kisha vipindi hivyo visambazwe kwenye vyombo vyote vya utangazaji na vituo vyote vilazimishwe kurusha vipindi hivyo kwa lazima tena virushwe bure!.
- Makala elimishi kuhusu kujikinga na Corona, ziandaliwe na kusambazwa magazeti yote na magazeti yote kuamrishwa lazima makala hizo zipewe nafasi front page.
- Kwa vile Corona haina dawa, hata huko kwenye vituo wanachofanyiwa wagonjwa wa Corona ni kusaidiwa na vifaa maalum. sisi Tanzania kwa umasikini wetu, level za maambukizi zikizidi we can't cope, Watanzania sasa wafunzwe tiba mbadala, ukimuona mtu mwenye dalili zaidi ya kumripoti, watu wafunzwe jinsi ya kujitibia kwa tiba mbadala, tutasaidia wengi kulikokutegemea kuwaripoti tuu. Kuripoti, turipoti yes, lakini pia watu wajitibu, tiba mbadala kibao zipo na zinasaidia kupunguza vifo!.
- Tutake tusitake ili kuliokoa taifa letu, lazima tifanye lockdown of some sort. Kati ya mikoa 25 ya Tanziania Bara na mikoa 5 ya Zanzibar Corona iko Zanzibar, Dar, Moshi, Arusha, Mwanza na Bukoba. Watu wa maeneo hayo wazuiliwe wasitoke kusambazia wengine na wale wengine, walio kwenye mikoa salama, wasithubutu kuja mikoa hatarishi kuifuata Corona.
- Productions houses zote tujitolee bure kutengeza vipindi vya uelimishaji umma kuhusu Corona, waandishi wa habari wakongwe turudi newsroomkujitolea kuandika makala, wasanii tutunge nyimbo za kuelimisha, yale magari ya matangazo ya burudani na wakatikaji sasa iwe ni kuhusu Corona, kila kitu ni kwa kujitolea, na hata wale dada zetu watoa huduma hizi na zilekipindi hiki cha Corona, nao pia wavae mask, huduma zao zinahitajika kama ilivyo kwa chakula, nao pia wanaweza kujitolea maana kiukweli kwenye Corona, pesa hakuna ni kujitolea, ila pia serikali nayo ifikirie kutoa stumulus package ya aina yoyote kusisimua uchumi maana hii bure bure kabisa mwisho wa siku badala ya wengi kufa kwa Corona, watu tutakufa njaa
Paskali