TBC na kipindi chenu cha Darasa Online, mnamfundisha nani?

TBC na kipindi chenu cha Darasa Online, mnamfundisha nani?

Ronee

Senior Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
155
Reaction score
155
Kipindi hiki kilibuniwa ili kuwasaidia wanafunzi ktk likizo yao ya muda mrefu iliyosababishwa na mlipuko wa janga la virusi vya corona.

Janga ni kama limeisha, wanafunzi washarejea mashuleni. huko mashuleni wanafunzi wako bize na waalimu wao kutekeleza ratiba za kila siku, na sidhani kama kuna utaratibu wa kuwawekea wanafunzi TV nyakati za vipindi.

Nauliza, je ninyi mnamfundisha nani? Kama mmeamua kutukumbushia wazazi enzi zetu tukiwa shule sina tatizo na hilo japo sidhani kama tunahitaji huo ukumbusho! Tena bora kipindi kingekuwa kinaenda hewani nyakati za usiku tungesema ni kwa faida ya wanafunzi wa kutwa.
 
Una wasiwasi gani wakati kodi ni zetu, acha warushe vipindi kuna wengine wakifundishwa pitia Tv wanaelewa zaidi kuliko mwalimu wake wa shule.
 
Unawasiwasi gani wakati kodi ni zetu, acha warushe vipindi kuna wengine wakifundishwa pitia Tv wanaelewa zaidi kuliko mwalimu wake wa shule.
Taifa lina mambo mengi yanayohitaji coverage mkuu, kwa muda wanaorusha vipindi hivyo ni obvious wanapishana na walengwa ambao kwa mida hiyo wanakuwa madarasani, TBC wanapaswa watumie kodi zetu vizuri kwa kuwa wabunifu. Bado tunahitaji kuwa nchi ya uchumi wa juu (donar country)
 
Sawa watakusikia mwana uchimu
 
Hili shirika sijui linakulaga maharage ya wapi.
 
Kumbuka kuna wanafunzi wa kutwa(Day Schoolars) sio wote ni wa Shule za kulala.!
 
Ronee,
Kuna kipindi cha mahusiano na nataka kutoka TBC TAIFA, hovyo kabisa.
 
Nauliza tu. Kwanini TBC hakuna ubunifu?
Sidhani Kama watu wanafanyiwa interview pale TBC. Pale mtoto wa mkuu akishafeli chuoni anaenda kutafutiwa nafasi pale. Kama ilivyokua NASACO. NASACO kulikua kumejaa ma failure watoto wa who,'s who. Matokeo yake Kila mtu anayajua
 
Kama hujaelewa hoja ya mleta huu uzi kaa kimya
Una wasiwasi gani wakati kodi ni zetu, acha warushe vipindi kuna wengine wakifundishwa pitia Tv wanaelewa zaidi kuliko mwalimu wake wa shule.
 
Una wasiwasi gani wakati kodi ni zetu, acha warushe vipindi kuna wengine wakifundishwa pitia Tv wanaelewa zaidi kuliko mwalimu wake wa shule.
Huo muda nao ni sahihi? Wakumbushwe basi wabadilishe mida wa kipindi
 
Kinasaidia sisi watoro na tunaotoroka shule break time.Tukifika nyumbani tunawasha TBC na mitihani tunafaulu.
 
Back
Top Bottom