TBC niwapinzani wa kuu wamageuzi ya nchi - katiba mpya

TBC niwapinzani wa kuu wamageuzi ya nchi - katiba mpya

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Nimeamua kuhama chanel sikutegemea chombo cha umma kikawa na ufedhuri na kumpuuza mtz kiasi hiki! Licha ya kongamano lenye kila sura ya kuamsha hasira ya mnyonge juu ya ubambucha wa chama cha ccm na serikali yake lakini kwamacho yangu tbc wameitangaza habari hiyo kama vile wameibia tu, yani ni kwa sekunde 15 tu huku wakimuonyesha jaji mkuu na akina cheyo na mvungi!!!
 
Unawatizama hawa bado! walianza vema na ungeweza kuwachukulia kama authoritative tv, kwa sasa wamebaki kushabikia siasa na hasa pale kina lipumba wanapoisema cdm, masuala ya msingi kwao sasa imekuwa si hoja.

Wamegeuka kuwa kasuku wa kutetea mafisadi, hii ni tangu walipojaribu kuuelimisha na kuuhabarisha umma kipindi cha mchakato majimboni na wakafungwa mdomo kwa mkurugenzi wao kunyimwa mkataba mpya bila sababu za msingi
 
TBC ni tv ya Mafisadi ukiiangalia nisawa na kuangalia Cartoon Network au ni bora kuangalia ngono kuliko TBC huta learn chochote zaidi ya Ufisadi. Hiyo tv inatakiwa kupigwa BAN na Invisible
 
kilio chao chaja na ikibidi tutawalamba bakora kwanza,wazandiki wakubwa na Mwenyezi anajua cha kuwafanya ...saa yaja watakuja kutubu hii dhambi kuu dhidi ya waja wa Mungu... tuwaombeeni!
 
hv siwezi kuwafungulia tbc kesi ya kunyimwa haki ya kupata habari ambayo ni haki yangu kikatiba? Coz hata mimi nachangia tbc kwa kodi yangu tena asilimia 14 ya mshahara wangu mbali na kodi ya bidhaa kwa hiyo kama mtz nina haki na uendeshwaji wa tbc na haki ya kupata habari sio kupewa habari ambazo hazina tija na kwa za manufaa ya mafisadi
 
Pole km bdo unaangalia Tbccm mpk leo! Cwapend wafnyakaz wte wa Tbccm! Wamepauka utafkr hawalipw mishahara na kodi ze2! Iko cku yao!
 
Kati ya vyombo vinavyotakiwa kusafisha baada ya katiba kubadilishwa ni TBC. Ni uozo mtupu hapo pamejaa unafiki mtupu ingawa wanalipwa na kodi zetu. ipo siku watajutia unafiki wao!
 
Ukijua sababu za kumng'oa Tido Mhando utajua tbc ni tv ya ccm!!
 
Kati ya vyombo vinavyotakiwa kusafisha baada ya katiba kubadilishwa ni TBC. Ni uozo mtupu hapo pamejaa unafiki mtupu ingawa wanalipwa na kodi zetu. ipo siku watajutia unafiki wao!

aliwahi andika Padri Karugendo ;TBC ni kero ya taifa,
 
Mmeshawasahau kipind cha kampen walipojika uhakimu wa kuamua kwamba haya ni matus na haya siyo
 
jamani unajua hata mimi nimeshanga sana hii tv ya ajabu sijapata kuona kuna mikono ya mafisadi ndani yake wameshindwa kuonyesha walichokuwa wanataka wananchi waende zao uko cha msingi ni wananchi wanajua wakombozi wao ni chadema tu na atutakaa tubadilike mpaka kieleweke
 
Uhuru, jambo leo, tbc fm, taifa, tbc1&2..hamna kitu...kwanza hii ni tv ya taifa cio ya ccm..how come maagizo ya how vioparate yatoke kisiasa?
 
Jamani muwe fair katika kuhukumu, taarifa ya habari siyo makala, ni kipande kidogo ambayo ni summary ya jambo fulani. Pale kila kitu kimeelezwa kwa ufupi na clips za watu muhimu zimewekwa, Jaji Samata. Shivji, Mkurugenzi wa kituo cha sheria na prof Maina na ujumbe umefafanuliwa na mwandishi. Sasa si inatosha jamani, najua mlitaka ipewe kipaumbele kwasababu ndiyo kiu yetu sote kwa sasa ila kwa habari inatosha ile tena clips zile zimezidi, mbona hata ITV wameonesha kwa ufupi mno kuliko TBC halafu hamsemi? ni kweli ni kodi yenu ila mkae upande wa taaluma yenyewe, ukiweka clips za muda mrefu utachosha watu.
 
Nimeamua kuhama chanel sikutegemea chombo cha umma kikawa na ufedhuri na kumpuuza mtz kiasi hiki! Licha ya kongamano lenye kila sura ya kuamsha hasira ya mnyonge juu ya ubambucha wa chama cha ccm na serikali yake lakini kwamacho yangu tbc wameitangaza habari hiyo kama vile wameibia tu, yani ni kwa sekunde 15 tu huku wakimuonyesha jaji mkuu na akina cheyo na mvungi!!!

Wewe ulitegemea nini? Kama Mchakato Majimboni uliondoka na mtu unadhani wakicheza na Mchakato wa Katiba si utaondoka na mtu pia!! Nani imvishe paka kengele? Sijui kama TBC ni TV ya Taifa, NIMEPOTEZA KUMBUKUMBU.
 
Back
Top Bottom