Ambayo hayapo kwenye tovuti ya mwanakijiji ni pamoja na haya:
1. Wadau wa Muafaka ni (CUF, CCM, Rais wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri na Mwisho Wananchi); sasa jiulizeni kama mwananchi angehusishwa je?
2. Kamati zilishakubaliana kwamba kamati hazikuwa na kauli ya Mwisho (Kauli za Mwisho zilikuwa zinatolewa na vyama,,, kupitia vikao vikuu vya vyama husika)
3. Makubaliano yoyote yalikuwa yatangazwe na makatibu wakuu wote wawili... (nothing go public unless there is a joint press conference with signed press)
4. Ajenga zilikuwa tano... nne tayari.
5. Agenda ya tano kukubalina Utaratibu wa utekeleza wa ajenga zote 1 hadi 4. Hivyo agenda ya tano ilikuwa haijaanzwa... so makubaliano yangekuwa wapi?
6. Kungekuwa na Makamu wa wiwili wa Rais, makamu wa Kwanza anatoka chama kilichochukua cha pili kwenye uchaguzi, na Makamu wa Pili wa Rais atatoka kwenye chama kitakachoongoza, yaani chama tawala... na makamu wa pili ndiye anaratibu wizara pamoja na kuwa mrithi wa Rais in case raisi akipatwa na jambo.
7. Kuwe na baraza la usuluhishe in case kama hakutakuwa na maelewano kati ya Rais na yule makamu wa kwanza wa Rais.
8. Kamati ya CCM ikapeleka maelezo ya hapo walipofikia... kama walivyokubaliana kwamba vyama ndio vyenye kauli za mwisho.
9. Halimashauri kuu inakubaliana na haya
i. Agenda zote nne zilivyozungumziwa. hivyo walikubali serikali shirikishi.
ii. Setup ya Serikali ... yaani ile inaondoa waziri kiongozi... na badala yake kuwe makamu wa Rais.
10. Marekebisho... Mapendekezo ya NEC.
a.. Marekebisho kwenye ile ya chama kushirikishwa kwenye baraza iwapo itapa kura...5% za rais... badala yake... Rais atumie vitu vya baraza la wawakilishi ya vyama vilivyopata... maana waweza pata 5% ya kura lakini usiwe na mwakilishi.
b. Kukiwa na baraza la wawasuluhishi kwa kuamua iwapo makamu wa rais wa kwanza na Rais watakuwa hawakubaliani... NEC wakasema... vyama ndio viwe wasuluhishi... nendeni mkazungumze na wenzenu (CUF) muelewane juu ya hilo.
c. Uratibu uliopo tulioridhi kutoka Uingereza ni ukishinda hata kwa kura moja unapata vyote,,, ukikosa kwa kura moja unakosa vyote... ndio utaratibu tulioridhi... Utaratibu huu maarufu unafanya kazi nchi nyingi... lakini ukweli haufanyi kazi Zanzibar... kwa sababu ya historia ya Utumwa, Matabaka, watwana, waungwana na kulikuwa na mgawanyiko mkubwa huko nyuma... hivyo kulizuka chuki na kutoaminiana tangu siku nyingi. Chaguzi zote za Zanzibar isipokuwa ya 1957 hizo zingine zote kila aliyeshindwa alikataa kushindwa... Kwa kuwa utaratibu wa Serikali shirikishi ni mfumo mpya kabisa wa Siasa Zanzibar. Basi pendekezeni namna ya kutekeleza hilo ili ifikapo uchaguzi unaofuata... utaratibu mpya utumike...
11. Haya ni maelezo tu ya ziada..
Matatizo yake ni:
- Historia,
- Kuwepo vyama viwili tu na vinavyokaribiana.