katika kuelekea uchaguzi october 2010 shirika la utangazaji TBC1 wamezidi kutoonyesha usawa wa demockasia kwa vyama vyote. kampeni zilipofunguliwa 20/08/2010 kila ulipofungua TBC unakuta rangi za kijani(CCM), siku zikaenda CUF wakafungua kampeni zao na wenyewe wakaonekana live and Chadema wakafungua kampeni wakaonekana live pamoja na kuwakatia matangazo.
Taarifa ya habari ya tarehe
27/08/2010 baada ya chadema kuzindua kampeni zao walionesha, CCM na CUF walioneshwa pia.
28/08/2010 CCM walionesha kampeni kwa mgombea wa urais, makamu, wabunge na madiwani, CUF walionesha mgombea urais tu CHADEMA ilikula kwao mana mgombea wao alikuwa DODOMA hakuoneshwa, je reporter wa TBC hawakuwepo?
29/08/2010 CHADEMA walionesha mgombea urais(lakini taarifa ilikuwa inakatika katika, wakaomba samahani ikaja kurushwa saa 4 watu wanaelekea kulala)
29/08/2010 TBC walionesha usawa kwa wagombea wote
30/08/2010 TBC walionesha taarifa za chadema zikiwa mgombea ubunge zikiwa zinakatika katika wakaomba samahani wakarudia sa 4 watu wakiwa wamelala, kwani TBC frequency zao zinabadilika wakifika taarifa za chadema?
02/09/2010 80% ya taarifa ilikuwa CCM, CUF walionesha mgombea urais na Chadema mgombea urais, hapa usawa uko wapi?
Muda katika taarifa ya habari ya jana 02/09/2010
Mgombea mwenza CCM dk 4.02.025, hapa aliongea mara 3 tofauti katika taarifa moja
Mgombea Urais Chadema dk 2.25.40 mgombea aliongea mara moja taarifa ilikuwa inabreak
Mgombea wa CUF alioneshwa mara moja
Mytake :TBC kwa sasa imenunuliwa na ccm
1.Inakuwaje TBC wanakuwa wabaguzi kiasi hiki?
2.Kwani ikifika taarifa za chadema frequency ya TBC inabadilika?
3.kwanini TBC taarifa zao za habari 80% ni CCM?
4.Reporter wa TBC wanafanya makusudi kutotoa ujumbe kamilifu kwa umma wakiogopa kufukuzwa kazi?