TBL na Serengeti Bia


Hizo ni dalili kwamba TBL wameshindwa Vita ya ushindani na SBL.Cha msingi wakae chini na kujiuliza ni wapi wamekwama/wameshindwa badala ya kutumia hizo MBINU CHAFU kabisa ambazo haziruhusiw/hazitakiwi katika USHINDANI HURU wa kibiashara(kama vp wabadilishe watu wote wa kwenye vitengo vyao vya masoko maana waliopo tayari wameonesha kushindwa,wameshindwa kuitumia elimu yao/wanaidhalilisha TAALUMA yao kwa kutumia MBINU chafu kama hizi,hao akaina SHELUKINDO&co waondolewe,wawekwe wengine) otherwise hawatafika mbali,SBL itazidi kupaa na kupaa na wao(TBL) watazidi kufulia....Taratibu naliona ANGUKO la TBL
 

Labda wazee wa media advertising watuletee gharama za kutoa tangazo hilo full page ya Mwananchi. Kweli wenye baa walipe pesa?????? Kwa uchungu gani while on the ground, Serengeti is the leading selling beer brand now? Hata sisi wanywaji tunalitambua hilo, nenda kakae kaunta jaribu kumpeleleza mtu wa kaunta ama hata mhudumu uone. Utasikia Serengeti na Tusker! Na hili ndo linawaumiza vichwa Makaburu kwani soon Tusker nayo itakuwa chini ya SBL, patamu hapo!
 

Hosea achana na Mwakyembe komaa na hawa Makaburu wa pale Ilala!
 
Wakuu,
Nimemaliza kusoma malalamiko (kutapatapa) kwa "Wamiliki wa Baa" na tangazo lao. Kimsingi ni utoto tu unaowasumbua TBL, kudhani kwamba wanaweza kuwahadaa Watanzania kwa mamilioni, kwamba waliotoa tangazo hilo ni wamiliki wa baa. Kuna masuala kadhaa nimeyaona katika tangazo hilo!

1. Wamekwepa kabisa kugusia kwa undani kiini cha tatizo ambalo ni ushindani usio wa haki, mwisho wake wamebaki kuongelea ushindani wa Pepsi na Coca Cola kila aya, wametoa hoja dhaifu mno za kujitetea. Hoja za majokofu yasiyo na vinywaji vya SBL kuwa ni hasara dhaifu mno!
2. Watoa tangazo (wamiliki wa baa) hawajaweka anuani zao wala baa zao ambazo wanadai wanazitetea, ili tujue ukweli ulipo. Hakika mimi ningeenda ktk baa hizo. Suala la kila baa kuwa na wastani wa matangazo 44 kila moja si la kweli kabisa, nikichukulia mfano wa baa kubwa 5 maeneo ya Mwenge na Sinza
3. Promotional materials zinazowekwa katika baa zao zinatoka makampuni yote ya vinywaji, lakini wao hawaliongelei hili suala kwa uwazi zaidi ya kulalamika kwamba SBL hawawapi hizo materials, kitu ambacho si kweli kabisa.
4. Jirani zetu Wakenya wametukanwa bila sababu za msingi (kama kweli zipo), kwamba walikuwa wanauza bia zenye kondom zilizotumika (kipengele namba 3, aya ya 2). Kwa hoja hii, kwa nini bia hizo chafu wasingezifikisha polisi ili wahusika wachukuliwe hatua.

TBL wanapaswa kujua kwamba Watanzania tumeelimika, hatuwezi kununuliwa kwa hoja zisizo na mshiko km ilivyo katika tangazo lao la leo, ambalo wametumia jina la WAMILIKI WA BAA (ambazo hazijatajwa majina popote katika tangazo hilo, wala zilipo katika Jamhuri hii)
 
tena wanatumia lugha chafu kwenye tangazo mi nawashauri sbl wafikishe tena suala hili kwa FCC na baraza la habari la taifa kwa vile tangazo linachochea vurugu na kuhatarisha amani. na kwa hili tangazo hawa wenye baa ndio wamkubali kabisa na wamethibitisha kununuliwa.

hebu tujiulize hawa wenye baa mbona hakuna logo ya chama na mwenyekiti hajasaini tangazo? huu si uhuni tu? kwanza nasikia huu muungano ni wa baa za ilala tu maana mimi rafiki zangu wana baa mbezi beach na hawamo! na nasikia member ni 70 tu sasa dar peke yake tuna baa na vioski kama 4000...hii ni asilimia ngapi? si ni hawa tu ambao ndio wamenunuliwa?

jamani tuamke SBL msikate tamaa piganeni hii ni vita
 
halafu suala la kibo leo nimebahatika kuongea na jamaa wa kibo zamani, hebu tuangalia KIBO imeuliwa na nani? TBL au EABL?

TBL walipewa KIBO na wakaiua within 24hrs watu wote SBL ikawachukua hii haikuwa kampuni ya kenya, wanatapatapa.na wakati huo kina mareale wlikuwa wanaongoza kuchafua bia za kibo na kuweka condom na vitu vichafu kwani nani hajui

wamefilisika kifikra na nawaonea huruma hawatafika mbali...ila hili la tangazo ni uvunjifu wa amani mbona hao waliotoa tangazo wasijitokeze front
 

Tupe data mkuu, mbane huyo ex-Kibo akupe data za kutosha. EABL nao inabidi wa-react dhidi ya hizi kashfa!
 
Nami pia nimelisoma the Guardian la leo lina hiyo press release ya Bar owners. Kwa mtazamo wangu ni kuwa pamoja na ukweli wa ushindani but sitafurahi sana kufanya biashara na wakenya (have shares on Serengeti).Huwa wanatuchukia sana na hawana mapenzi mema kwa Tanzania.

Na ninakuhakikishia kuwa the so called East Africa Cooperation (Tz, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi) haitastawi. Nina uhakika huu. Niliwahi kuwa Kenya kwa Muda, Wakenya hawataki kabisa kuona Tz inafurukuta, tena from the high authority perspective!!!

At the sametime, hatutakaa tufaudike na huu muungano wa nchi 5. Tena tusipokuwa makini tutapoteza amani na uhuru wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…