TBL wamepandisha bei ya bia kabla ya Julai mosi, hii ni halali kweli?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Wakuu wana JF,

Nasikitika kuwataarifu kuwa TBL wamepandisha bei ya bia kwenye maeneo yetu kabla hata ya siku iliyopangwa kwa madai kuwa serikali imepandisha kodi.
Hivi sasa bei ya kreti ya bia inauzwa 32000/= badala ya 28500/= ya zamani.Jana kwenye depot zao hawakuuza bia kisa serikali imepandisha kodi.Hivi sasa chupa moja inauzwa 2200/= badala ya 1800/=.

Kwa nini sasa wanapandisha bei kabla ya muda wake?
Kwa wanywa pombe mnapaswa kugoma kunywa.

Nimeayajua haya baada ya kutumwa kwenda kununua pombe za harusi ya ndugu yangu.
Maoni yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…