Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Kampuni ya bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro imetoa udhamini kwa timu mbili maarufu za SIMBA na YANGA...Udhamini huo ni wa miaka mitatuambapo kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu kila timu itapatiwa Tshs.millioni 654 kwa ajili ya uendeshaji wa klabu,mishaara ya wachezaji na viongozi wanaoambatana na timu,usafiri wa timu,vifaa vya mazoezi,matangazo nk
Hivi jamani Simba na Yanga mpaka lini????,why not Mtibwa Sugar,Moro UTD,Villa Squad,Polisi Dom,Prisons au timu nyingine zaidi ya timu hizo mbili ambazo hazisaidii lolote ktk kukuza soka la Bongo,,,halafu mbona tayari Yanga wanaye Manji!!!!!TBL wateja wao wakubwa wako mikoani so wajitahidi kuzisaidia na timu za mikoani pia ambazo zinahitaji wadhamini kwa udi na uvumba....makampuni yajaribu kubadilika na kuziangalia timu za mikoani pia