TBS hamjui mnachofanya

TBS hamjui mnachofanya

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
271
Reaction score
484
Ndugu zangu naomba nichukue nafasi hii kupeleka lawama katika shirika la viwango Tanzania.

Hawa watu niwazee wa media pale wakipata kitu kisichoruhusiwa kutumika basi wataita vyombo vyote vya habari kujifanya wanafanya kazi waonekane, but ukweli hawa watu wapo wapo tu.

Fikiria mtu unaingiza si chini ya container tano kila mwezi, TBS wanakwambia mzigo usiuzwe kama hawajaja kuchukua sample, yes tumekubari, hata kuja hawaji inaweza kuwachukua mwezi na zaidi kuonekana, hapo unadhani kama mfanya biashara utakuwa katika hari gani?

Kuna wakati unakuwa na back order za watu na ushawaaminisha wanazipata katika wakati rakini you make them wait for a month or two! Unapoteza imani kabisa.

Jambo lingine ni wizi wa wazi unaofanywa na hawa watu, sample ya oil mtu anataka dumu la lita 20 lote la nini? Nnavyojua hata robo lita haifiki inayoenda lab.

But jambo la msingi ni HAWA WATU WANAINGIZA WATU KWENYE HASARA KWA KUTOFANYA KAZI KWA MUDA, HATA UKIWAPIGIA WAJE KUKAGUA HAWAJI.! SHAME ON YOU TBS
 
Wachane tu maana tulishachoka na taaluma zao feki na vyeti feki, kila kitu hawawezi, wakishughulikiwa wanadai nchi inaongozwa kidikteta, kumbe wao ndiyo wamekaa kibwanyenye(mabepari+wezi wa kalamu).
 
Back
Top Bottom