TBS YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA KOROSHO (WASINDIKAJI NA WAFUNGASHAJI) - MKOANI LINDI
Na Mwandishi wetu Mkoani Lindi;
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi zingine za serikali leo Tarehe 13 Septemba, 2021 wanatoa mafunzo kwa Wajasiriamali wapatao 40 ni Wasindikaji na wafungashaji wa korosho na bidhaa za korosho.
Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Terack. Pia Mkuu wa Mkoa ameipongeza TBS kwa maandalizi mazuri ya mafunzo hayo muhimu na niombe utaratibu wa mafunzo kama haya uwe endelevu.
"Natambua mafunzo haya ni uthibitisho wa azma ya Serikali kupitia taasisi zake katika kufanikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati kupitia Uwekezaji katika Viwanda na hivyo kuuza bidhaa zitokanazo na korosho nje ya Nchi" - Mhe. Zainab Terack (Mkuu wa Mkoa wa Lindi)
Mafunzo watakao patiwa Wajasiriamali hao kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi zingine za serikali kama SIDO, mafunzo hayo yatajikita katika maeneo yafuatayo;
1) Viwango na matakwa ya Viwango vya korosho
2) Kanuni za kilimo bora
3) Kanuni bora za usindikaji
4) Usajili wa Biashara
5) TeKnolojia mbalimbali za usindikaji korosho na bidhaa zake
6) Vifungashio na ufungashaji wa bidhaa za korosho
7) Upatikanaji wa korosho ghafi na korosho katanga
8) Utaratibu wa kuthibitisha ubora wa bidhaa na usafirishaji wa bidhaa kwenda nje ya Nchi.