OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
NAIBU Waziri Mkuu, Dk. Dotto Biteko, amesema Tanzania ina umeme wa ziada wa Megawati 740 na kwamba katika serikali ya awamu hii ya sita inakwenda kukamilisha mipango yake ya miaka mingi ya kuuza umeme nje ya nchi.
Dk. Biteko ambaye ni waziri mwenye dhamana ya Nishati, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua maandalizi ya Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), utakaotumika katika mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuanzia Januari 27 na 28 mwaka huu.
Alisema tayari maandalizi kwa ajili ya kuanza kuuza umeme huo yameanza kwa kujenga laini zitakazotumika kusafirisha umeme huo kwenda nchi jirani ikiwamo Zambia.
"Nchi yetu tunao umeme wa ziada, kwa mitambo yetu yote tuliyonayo tukijumlisha, tuna zaidi ya megawati 740 ambayo ipo tu ambayo tungeweza kuitumia kama tungekuwa na mahali pa kupeleka," alisema Dk. Biteko.
"Lakini hatuwezi kupeleka huo umeme kwa wenzetu kwa sababu hatuna njia za kuwapelekea. Kwa mfano Zambia, wana changamoto ya mgawo wa umeme kwa muda mrefu, kwa sasa tunajenga laini ya kutoka Iringa, Mbeya kwenda Tunduma, baadaye tuunganishe na wenzetu wa Zambia, na tayari tuko kwenye hatua za mwisho majadiliano ya kuwauzia umeme.
"Ile ndoto ya mliyokuwa mkiisikia kwamba tutauza umeme kwa wenzetu, imesemwa kwa miaka mingi, inakwenda kutokea kwenye awamu ya sita ya serikali. Tayari mikakati hiyo ipo, tumeikamilisha, hivi ninavyozungumza tumeshajiunga na wenzetu wa Kenya, Burundi na Rwanda kupitia mradi wa Rusumo, wakihitaji umeme hata jana tutawapatia," alisema Dk. Biteko.